The Chant of Savant

Sunday 12 September 2010

Tishio la kuchoma Qur'an ujuha na wendawazimu..






























Mwezi wa Ramadhan umeisha katikati ya kitatange cha mchungaji mmoja mchumia tumbo Terry Jones wa Gainesville Florida nchini Marekani alipotishia kuchoma nakala zipatazo 200 za Qur'an. Jambo hili lilizua maandamano kwenye nchi mbali mbali za 'kiislam' ikiwemo nchi iliyoshindwa ya Somalia.

Wengi walijiuliza mantiki ya wasomali kuandamana kupinga tukio hili huku wakishindwa kuandamana kuwashinikiza mabwana vita walioliteka taifa hili wafikishwe mahakamani. Hii imenikumbusha kisa cha kipumbavu kilichotokea nchini Sudan mwaka 2007 ambapo mama mmoja mwalimu wa kiingereza Gillian Gibbons alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kuandika jina la Mohammad kwenye zawadi ya kinyago cha dubu alichompa mwanafunzi wake alyeitwa Mohammad.

Wengi wenye akili walijiuliza mantiki ya wasudan kuandamana wakiwa wameshikilia visu na mapanga kupinga 'kufuru' hii ilhali wasudan hao hao wakimkingia kifua ili asikamatwe na mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) muuaji Ahmad Harun ambaye jina lake Ahmad pia ni jina la mtume Mohammad! Wengi walizi kushangaa wauaji wengi wanaoendesha mauaji ya kimbari jimboni Darfur kuwa na jina Mohammad!

Hivi ni kina Mohammad wangapi wanakula unga, vibaka, wabakaji na mengine mengi?

Mambo yalizidi kunoga na kubainisha wendawazimu pale waandamanaji walipochoma bendera ya Marekani. Inashangaza binadamu tumekuwa majnun na wehu kiasi hiki! Tumeshuhudia bendera ya Marekani ikichomwa na wehu waliokuwa wakiandamana kupinga kuchomwa kwa Qur'an. Yaani unapinga jinai kwa jinai? Hakika huwezi kufua nguo kwa maji taka ikatakata.

Hivi kweli kuna mtu anaweza kuchoma Qur'an yaani ujumbe au ni kuchoma vitabu tu? Huwa najiuliza kati ya aliyehifadhi Qur'an na tabu Qur'an ni ipi? Huu ni ushahidi kuwa wengi wanaojiita waislam japo si wote ni washirikina. Kwani wanaiona Qur'an kwenye maandishi wakishindwa kuijua kwenye mitima!

Hivi ni hafidhi wangapi wanapanda dala dala na kukaa karibu na vyangudoa, walevi hata mafisadi? Ni ajabu kidogo!

Hakuna anayeshabikia kuchomwa kwa Qur'an sawa na kuchomwa bendera ya nchi yeyote.

Wengi bado wanajiuliza mantiki ya kujengwa msikiti kwenye eneo la Ground Zero lilipokuwa jengo la World Trade Center (WTC) lililolipuliwa na kufutwa toka kwenye uso wa dunia hapo Septemba 11, 2001 ambalo, maadhimisho yake ndicho chanzo kikuu cha mgogoro wa tishio lililositishwa la uchomaji Qur'an. Wengi wanaona kujenga msikiti kama ni kuwakumbuka magaidi, na kwa kiasi fulani, kuwakweza kwa kitendo chao cha kishenzi. Wengi wanahoji, ingekuwa Makka wangeruhusu msikiti kujengwa kuwakumbuka magaidi wa dini nyingine?

Wengi wangejua kuwa Jones alikuwa anatafuta namna ya kujulikana na kukuza kanisa lake la kibabaishaji dogo, wasingepoteza muda wao na kuonyesha wendawazimu dhidi ya kupambana na wendawazimu. Let a fool hold his tongue and he will pass for a sage.  ~Pubilius Syrus
Somo kuu hapa ni kwamba: tapeli mmoja, sawa na wale wa viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam na kwenye luninga, amefanikiwa kuwatumia waislam wapumbavu kupata umaarufu na kufanikisha lengo lake. Nia aibu iliyoje?

Tumalize kwa kuhoji. Je kama Jones angechoma Qur'an ingekuwaje? Je jua lingesimama au kudondoka? Ni ajabu kuona kitu ambacho hata mtume Mohammad hakuacha kuwahangaisha watu wakasahau hata kufikiri! Je Qur'an ina maana kuliko binadamu wanaouawa kila siku ilhali ilishushwa kuwatumikia si wao kuitumikia? Tutafakari tena kwa sana.Je Qur'an ambayo ni kifaa ina thamani kuliko binadamu?

Kituko na wendawazimu zaidi ni pale mwanasheria mmoja wa Australia Alex Stewart alipochana Biblia na Qur'an na kutumia karatasi zake kutengeneza msokoto kuona ni kipi kinaungu vizuri. Hii maana yake ni kwamba matepeli wengi sasa watajitokeza, sawa na makundi ya kigaidi, kuvichoma vitabu hivi wakitafuta kujulikana!

4 comments:

Ibrah Rahbi said...

Kwanza nilipoanza kusoma blog yako nilijua mzima kumbe kichaa hakuna shida unahoji kati ya qur-an na binadamu nani zaidi!! huwezi kujua nini zaidi kwa sababu huijui qur-an kifupi ni kafiri!

Jamal kishangu said...

Kweli unajua kupayuka

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ndugu Ibrah Rahbi
Shukrani kwa kunitembelea na kusoma. Nadhani unajua kuwa kila mwanadamu amepewa akili aitumie atakavyo chini ya haki na uhuru wa kutoa mawazo yake. Nilitegemea ungejibu hoja badala ya kutoa hukumu na kashfa. Heri mimi ni kafiri kuliko wewe asiyefikiri.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ndugu Jamal Kishangu
Shukrani kwa kupitia hapa na kuacha unyayo. Nazidi kukukaribisha usiache kupita na kuacha unyayo. Siku hizi sipayuki bali nafyatuka na kufyatua kila jumatano kwenye gazeti pendwa la Mwananchi. Karibu