The Chant of Savant

Wednesday 29 June 2011

Hongera wanakijiwe kwa tuzo la kimatatizo

BAADA ya kurejesha namba kwa mtabiri aliyekuwa akitumiwa na wanasiasa kuwatisha walevi, mzee mzima nimeamua kuanza kutabiri.

Sitakuwa nikitabiri kila siku. Siwezi kufanya hivyo hadi nipate ujumbe kutoka kwa aliye juu. Msiulize juu wapi na juu ya nini wala nani.

Pia nitoe onyo. Wale waganga njaa na wasanii wa kisiasa wanaoingia kwenye madaraka makubwa kuliko uwezo wao ili wayatumie kuwaibia walevi kama ilivyo wasipoteze muda kuja kuomba niwabebe kwa kutoa utabiri wa vitisho.

Mie naaminika kwa uhakika wa utabiri wangu tofauti na tapeli yule marhuni. Sitabiri kutisha watu wala kuwafurahisha wezi wala nini bali ukweli mtupu. Isitoshe mie siendeshwi na tumbo kama wao bali nguvu za Aliye juu. Hayo leo hayanihangaishi zaidi ya hizi tuzo za kisanii na kufuru zionyeshavyo wenzetu wanavyotuona mataahira wa mataahira kulaleki!
Chanzo: Tanzania Daima Juni 29, 2011.

Utabiri wa leo ni mchaganyiko. Kwanza niliota kuwa baadhi ya wezi wenye mamlaka watakwenda Nyuyoko kupokea tuzo feki ili walipane per diem kama mlivyoshuhudia wakikenua kama vyangu. Hapa namaanisha kina Geib Bihalali na Stivi Wahasira ambao walionekana kule wakikenua kwa usanii. Eti Bongolaland imenyakua tuzo! Ama kweli watasha wamejua kututenda!

Kwa vile sasa hii ndiyo sera mpya ya jamaa zangu wasanii, tukubaliane kuwa wamenyakua tuzo. Sasa naanza kutoa utabiri. Baada ya kunyakua tuzo ya hujuma bora za jamii, Bongolaland itaanza kung’ara kuliko mataifa mengine duniani.

Najua kuna mijitu itaguna kuwa hakuna huduma bora bali bora hujuma. Hivi hii mijitu inayoguna haioni watoto wanavyokaa juu ya mawe mashuleni ili kuokoa miti? Haioni jinsi wajawazito wanavyopelekwa hospitali kwa bajaj ili kuepuka kuchafua mazingira? Anayebisha aende pale Mwanamanyala aone wanavyotendewa kwa ukalimu bila rushwa wala kuwaacha na mikasi kwenye matumbo ukiachia mbali kuokoa vichanga vingi visifie getini kwa kukosa ngawira.

Pia Muhimbili ni mfano bora ambapo madaktari waliwahudumia vyema wagonjwa hadi wakachanganyikiwa kwa furaha na kuwa vichaa kwa muda kiasi cha mmoja kumnyotoa roho mwenzake ukiachia yule aliyepasuliwa kichwa badala ya mguu akadedi kwa furaha ya huduma bora.

Hivi jamani hamuoni wajawazito wanavyoteswa, watatu kitanda kimoja ili kubana matumizi ya kununua vitanda? Kuwabanisha wajawazito kitanda kimoja kunajenga mazoea kwa watoto watakaozaliwa kujua kubana matumizi. Asiyeona hili ama ni chizi au kipofu.

Hebu nipigieni makofi kidogo kwa kufichua neema hizi. Nani hajui kuwa kupunguza vitanda kunaongeza mashangingi ya wakubwa? Je, hizo si hudama bora? Tuendelee.

Hivi hamuoni mvua ikinyesha jiji la Bongolalalandcity linavyojaa swimming pool za bure na pafyumu ya bure? Hivi hamjui kuwa wabongolalalanders wameshiba huduma za jamii na kutosheka kiasi cha kuwapenda viongozi wao hadi watawala hata nusu watawala, wake, watoto hata waramba viatu wao wakipita barabara zinafungwa ili wapite bila usumbufu?

Uzuri wanafanya hivyo bila kujali kuna mgonjwa au wanaoungua kwa jua na vikwapa kwenye madala dala. Huo ndiyo uongozi bora na huduma bora za jamii ati.

Funga kazi ni kutumia giza badala ya umeme ili kuepuka utumiaji mbaya wa nishati. TWANESKO upo mshirika hapo?

Kwanza tuzo hii itageuzwa sera na majasifu kutokana na watakaofanya hivyo ima kuishiwa sera au kujulikana wasivyo na sera wala akili. Sitawataja mnawajua. Natatibiri kuwa kesho mtasikia Bongolalaland ikinyakua tuzo ya utawala bora hasa kutokana na sera yake ya bora utawala chini ya kisingizio na ngonjera za utawala bora.

Maana duniani hakuna utawala bora kama ule unaoweza kuamrisha geshi la manjagu likanyonga walevi na hao mabwana zake wasikemee kama walivyofanya kwa kaka Moi Kibaka. Bongolalaland ina kila sifa ya kupewa tuzo ya utawala bora kutokana na utawala wake kuzingatia kujuana, mitandao, familia, ufisadi, ufisi na usanii. Rafiki yangu Njaa Kaya na Riz two mpo hapo?

Siku hizi licha ya kuficha watu unaoandamana nao kwenda kutanua, naona mshirika wako wa bedroom amegeuka ama waziri wa mambo ya ughaibuni au makamu wako.

Maana ukienda popote ukiongoea na dingi naye anaonyeshwa akiongea na maze. Siri ya mafanikio haya yote nini? Utawala na u-twawala bora. waleni walevi kama hataki kustuka.

Baada ya hapo tutegemee tuzo ya kutunza na kupamba ufisadi. Hapa kigezo cha ushindi itakuwa ni jinsi tulivyoanzisha na kushughulikia HEPA na Richmonduli ambapo kaya ilipata faida na maendeleo ya kutisha hasa kwenye medani za siasa.

Baada ya tuzo hilo hapo tegemea jingine la kuthamini wageni kuliko walevi bila kusahau ukarimu.

Tuzo itakayofuata baada ya ile ya kutunza na kupamba ufisadi ni ile ya kutunza mito hasa kule mkoani Mara ambapo juzi juzi kulikuwa na maandamano nchini Kanada ya kuunga mkono kuchanganya tindikali na maji kiasi cha kuwageuza wabongolalanders wazungu.

Nani mara hii amesahau yale maneno yaliyosikika mwekaji mmoja akimtishia mwenyekiti wa kijiji kuwa apokee mshiko baada ya kumwambia kuwa hata rahisi anahongwa itakuwa yeye.

Jamaa aliyesema hivyo nasikia anatokea kule Ukanada na anaitwa Mr Jeff. Anyway nikienda Ukanada nitaongea na bwana Harper. Maana tulisoma wote kwenye chuo kikuu cha Calgary. Hayo ni masuala binafsi tuyaache.

Tuzo zinaendelea kumiminika. Tuzo itakayofuata ni ile ya polisi kuwakomesha viherehere na kuwalinda wawekaji. Nani masahau yaliyotokea kule Tarime ambapo manjagu waliwakomesha walevi waliokuwa wakitaka kukomesha uchanganyi wa maji na zebaki wasijue ndiyo maendeleo. Njagu walinyonga sita bila taasisi za kimataifa za haki za binadamu hata kujali. Taasisi hizi huwa hazishabikii upinzani. Tuyaache.

Tuzo itakayofuata, natabiri. Itakuwa ni tuzo ya uwekezaji bora unaolenga kukuza chumi za watawala huku ukidumaza uchumi wa walevi. Leo sitaki nifumue balaa hili.

Give me some times somewhat in he future, I will try to explain this usufunctuary like rights of the walevi to benefit from their country.

So too, I surely will dwell on the whole fiasco whereby the venal rulers are stealing in the broad light day. What a heck! Sorry. Mwenembago alipanda nikaongea kitasha.

Tuzo funga kazi itakuwa ile ya watawala kutanua huku walevi wakipukutika. Please give more time for research.

Hivi yule manzi hawezi kuwa tuzo yangu tonight? Ngoja nimuwahi ili nipate tuzo ya ujogoo. See you all.

2 comments:

Jaribu said...

Inatia uchungu hali ya Tanzania. Badala ya kuikabili hali ya nchi sasa hivi, serikali ya vilaza wenye Phd feki au za kugawiwa wanaanza kumgeuzia kibao Nyerere utafikiri kuwa ndiyo anayeongoza nchi sasa hivi. Ni very apropos unavyozungumzia mambo ya tuzo, kwa sababu hiyo ndio wanajua. Tuzo ya urais, tuzo ya International Chamber of Commerce, tuzo ya BAE. The only tuzo wanayomiss ni ya competence.

30 June 2011 05:49

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu, I cannot hold my laughter though it is painful. What? Tuzo ya competence? Guy go give that tuzo to the nyani for doing its unyani competently.
Thanks for visiting us quite often.