The Chant of Savant

Wednesday 10 August 2011

Mpyayukaji the kila kitu

Ninarap ninarap ninarap

Nawakilisha mistari, ninarap

Machizi wanapagawa ninarap

Kama sina akili nzuri, ninarap

Yo yo yo yo ninarap

Nami siku hizi siachwi nyuma. I am Mpayukaji the jack of all trades so to speak. Acha nimwage ung’eng’e kuonyesha mie si kilaza kama Makambale au wale vilaza walioghushi PhD. Hamkumsikia mmojawapo aitwaye Diddy Masemburi akilalamikia waishiwa baada ya kumvua nguo kwwenye dili la UDA? Ajabu eti kilaza mwenzake Makorongo Muhanga anaamua kumtetea bila aibu asijue tunawajua walivyo vilaza walioghushi PhD! Siku hizi kila mtu, hasa matapeli, anapenda kuitwa dokta kama wafanya mazingaombwe.Hayo tuyaachane nayo ingawa yanatuathiri hasa sisi walevi wa Danganyika.

Pamoja na kuwakilisha mistari kuonyesha kuwa mie ni The Kila Kitu yaani TKK, nataka nitoke kivyangu vyangu na mistari yangu hapo juu. Sitatoa mistari mingi kuogopa wezi wa sanaa kuniibia mistari na kuanza kuwa masupa staaa hata kama ni wachovy wanuka jasho wa Danganyika. Kwa ufupi, ni kwamba kwenye mambo ya Uongofleva nimo kinomanoma nikimwaga mistari. Nawakilisha kama sina akili nzuri.

Kuonyesha ninavyoyanyaka ma-Uongofleva, nimetoka na minyororo mikubwa kuliko ya mbwa shingoni. Sorry si minyororo. Ni cheni. Hata kama ni za shaba na mawe na si dhahabu na almas. Bling bling ni bling bling hata kama ni ya mbao. Kwani niko peke yangu? Hamuoni hata wanaoitwa waheshimika wanajinoma mibling bling kwenye vidole masikio hata makalio kama yule mbunge machachari, Sonko wa kule kwa mzee Moi Kibaka sorry Kibaki? Hata bi mkubwa mwenyewe anajinoma kama hana akili nzuri. Mzee mwenzangu Dugong Ben wa Nkapa huwa hatupi mnyororo shingoni. Je hapa mtasema mie mbwa au mheshimika kama Dugong?

Ngoja nizidi kuwamegea. Nimetinga suruali ililyolegezwa hadi chini makalioni au sagging kwa kimanga huku nikidunda bega moja juu jingine chini kinoma. Mkononi nina justice au elephant. Wasiojua elephant au justice ni msoba au tuseme sigara kubwa. Nasema kimoyo moyo bangi nibangue nimwage vitu.

Kwenye masikio nimetinga mihereni kibao kuliko hata akina Ole. Japo natukanwa eti mtoto si riziki kwa kutoboa masikio, najifanya hamnazo hata sijali. Nadunda mwendo wa Dola si ndururu. Si juzi baba mdogo akasema eti atanitafutia mume aniozeshe! We palitaka kuchimbika bila jembe kama si mzee mwenyewe kuingilia. Hayo tuyaache ni ya wale wanaotuona limbukeni wakati tunafaidi fasheni za majuu zinakwenda na wakati. Mbona P Daddy anaweka vitu kama vyangu? Mbona akina senti 50 nao wanafanya vitu kama vyangu. Mungu akupe nini duniani, kuvaa kama mtasha hata kama unaishi kwenye kiza cha mgao? Hata kama hatuishi kama watasha bado tunafaidi na mapozi yetu ya mende. Heri yangu nimetoga masikio kuliko akina supastaa uchwara wanaofuga vichiwawa au vijibwa vidogo vidogo. Mie nikaamua kufuga dog nitafuga Germany Shepherd au Labrador Husky. Wasiojua aina hii ya mbwa ni kama ile aliyokuwa amefuga Bill Clinton. Na chiwawa ni kama yule wa Joji Kichaka. Upo hapo chizi wangu? Mie ni mchizani wala simlaunguwi mtu wese wala kuiba Uda? Mpo hapo majambawazi wenye nazo walanguzi na wala na watoa rushwa?

Ngoja niwakoge washamba hata kama mimi ni limbukeni. Kila nikipita mitaani naangalia huku na kule kuona kama kuna watu wananiangalia super star mie. Wengine wanakandia kuwa eti mimi ni super star uchwara. Mara utasikia wakisema: super star mwenyewe apeche alolo na alikimbia shule.

Nimepiga pamba zenye chata babu kubwa wafikiri maneno yenu yatafanya niache ulimbukeni? Siku hizi ulimbukeni unalipa. Waulize wahishimiwa wanavyomwaga ung’eng’e uchwara au tuseme kiswanglish wakiwaingiza wale wa kwa mama wasijue wale ni lugha yao! Je hawa nao si limbukeni?



Naingia na uongofleva kuwaibia malimbukeni waliojaa kayani. Nawapa vipande kupitia mistari lau waamke na kuacha ulevi na ushamba. Badala ya kushabikia upuuzi kama kitchen party na kuchangia harusi waanze kujenga mwamko wa kimapinduzi wa kuborosha maisha yao.

Kwa vile mie ni The Kila Kitu jiwe gumu, napanga kufanya kila sanaa lau niukate kama akina Roast Tamu, Ewassa, Endelea Chenga hata Riz-One. Kwa hiyo, msishangae kusikia mipango na mikakati yangu.

Juzi nilipita sehemu nikaona maajabu. Nikiwa nawaza kujifanya mtangazaji wa runinga bambataa si nikakuta CV ya mfala mmoja limbukeni mtangazaji anayepayuka sana pumba. Sikuwa najua kuwa jamaa ni Kilaza bin Kihiyo. Kumbe jamaa aliondoka na divisheni ziro kwenye mtihani wa kidato cha nne! EF Kivalley upo hapo? Ajabu kesho utasikia jamaa ana Masters na baadaye PhD kama za jamaa zangu walioshukiwa na Keine Mlongakweli. Hapa akina Billy Lukuveee, Chitaahira, Merry Nangu, Makorongo Mahanga, Diodorant Kamara, Emmy Nchimvi, Mwambalaswai, Chengeni,Diddy Masab—uri na wengine wengi ambao kughushi kwenu hakujafichuliwa mnaninyaka. Baada ya kugundua kuwa kumbe Kivalley ni kibonde kweli kweli nimeamua kuwa mtangazaji wa runinga. Nitaanza kubwabwaja kama sina akili nzuri. Ili kuwavutia walevi nitakuwa nacheza miziki ya X maana najua wanapenda mambo X X. Hata akili zao Mungu keshaziwekea X. Kila kitu kwao ni X kama nyumba zilizopangwa kubomolewa huku wahusika wakipaisha malipo. Wataacha kuiibia mijitu yenyewe kama ni hovyo kiasi hiki? Hayo tuyaache. Wenye vituo vya runinga jiandae kupata kifaa mithili ya mzee mwenyewe Larry King. Mie nitakuwa nikitumia jina la Larry Dog King Kong. Haya tuyaache. Ukifika wakati wake nitadurusu zaidi jinsi ya kutengeneza mchicha kama wale wachizi waliojitwalia UDA. Idd Lion upo? Nasikia uligaiwa madafu 250,000,000. Hii kweli imeniuma sana. Maana nilikuwa nikikuhusudu kwa utetezi wao wa uzawa kumbe uzawa wenye si mali kitu bali uliwa siyo? Mtu mzima hovyo.

Nimalizie na upande wa pili wa usupa staa uchwara. Juzi nusu mshirika wa bedroom ajinyotoe roho baada ya kutishia kunipa talaka kutokana na kumdhalilisha. Si nilikwenda nikachora tattoo mkononi ili nionekana kama akina Snoopy Dog. Nilitaka nibadilishe hata jina niitwe Big dog au mzinga wa mbwa. Pia nilitaka nianze kuimba muziki wa injili aina ya shamkwale.

Mama alizoza hadi nikatamani kujinyotoa roho kama siyo kuwahi kijiweni na kupata kahawa na tangawizi ambavyo viliyeyusha hasira zangu. Wale ndata mbona kama wanakuja huku! Ngoja nitimke kabla hawajanibambikizia kesi. Maana, wakitaka mshiko mie sina. Kulaleki!

Chanzo: Tanzania Daima Agosti 10, 2011.

2 comments:

Jaribu said...

Ha Ha! You are killing me! Since wabongo wenyewe wameamua kuwa kondoo inabidi tucheke tu, ama sivyo utapata presha ukifikiria nchi isivyokuwa na mwelekezo na watu wanateseka tu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hata ukiacha kuifikiria hii nchi isiyo na mwelekeo bado presha utapata. Wakati mwingine inabidi kujifurahisha huku ukiwafurahisha wengine. Muhimu jumbe iko fika na levi anza elewa.