The Chant of Savant

Tuesday 30 August 2011

Natafuta kijogoo cha kike kiniwowe

Haki ya nani mambo yanazidi kubadilika! Sijui haya ndiyo maendeleo, maanguko, kulipiza visasi au kusahihisha mahusiano ya jamii! I have no idea. Nani alitegemea mwanamama angeoa mwanarume tena wawili kwa mpigo? Anayedhani hizi ni rongorongo au pumba za gongo ameumia na atachekwa. Kama husomi magazeti kwa vile u kilaza au apeche alolo basi fungua masikio maneno ya injili ya mlevi yaingie. Imetokea openly and live. Are you thither? Usiniulize maana ya thither ingawa yaweza kuwa there au pale. Juzi si nilisikia walevi wakisema kuwa kule Mpanda ya Sumbawanga au Tupa uchawi, kuna mama kaoa walume wawili ambao wanamshea bila mitwalingo wala nini. Sijui wamepigwa limbwata wakingojea kahando au la. Mie sijui.

Huyu mother nimem-love kweli. Maana, baada ya kufanya usharmutah na kushindwa akaamua kufanya kweli. Heri yake ameamua kuchukua haramu yake kuliko makabila fulani yanayochukua kaka na dada na wajomba zao. Hayo tuyaache.

Hili la mama kuoa mibaba tena mibee si jipya. Juzi si mlimsikia yule balozi akifungua kampuni kwa jina la anayeonekana mumewe wakati ukweli ni mkewe wa kiume kule kwa Joji Kichaka.

Kwa vile kuna wanamama wenye ubavu wa kuweza kuwaoa warume, nami natafuta kijogoo cha kike kinioe lau naweza kuondokana na ukapa huu wa nanihii baada ya kuachwa na aliyekuwa wa ubani wangu. Najua viherehere weshaanza kusema eti mie ni mtoto si riziki. Hasha! Nataka kuolewa na kijogoo cha kike si cha kiume. Hivyo tuelewane barabara hapa tusijetoana nundu bure.

Hata hivyo nina masharti. Huyo kijogoo wa kike atakayetaka kunioa lazima awe tayari kuninyenyekea. Sitaki mama wa kunidunda au kuninyoshea domo hasa baada ya kuwa nimeutwika. Maana naweza kumnyotoa mtu roho bure nikaishia kunyongwa pasina ulazima. Najua kuna njemba zinazodundwa na wake zao. Ukikutana nazo mitaani zinavyojishaua. Juzi nilimsikia mmoja pale Uwanja wa Fisi akisema eti mwanamke hambabaishi wakati tunajua anakong’otwa na mkewe kama mtoto mchanga. Wapo wengine wanavishwa magagulo na kupiga deki tena vizuri ingawa hatuwaoni. Hata kama mimi ni mmojawapo yakuhusu nini? Mbona pale Kenya wababa walikimbia kwenda kuomba msaada baada ya kukunyugwa na akina mama yaani memsahib wao? Wadhani nchezo na uongo. Watu wanafanyiwa kweli sema hawasemi kwa vile nyumba zinaficha mengi. We ziache nyumba ziitwe nyumba.

Unakuta baba zima likikwidwa na halifurukuti kwa vile halina kitu. Linaogopa likipandisha Mwenembago mshirika wa bedroom atalitishia kuwa ‘nitagawa kama sina akili nzuri’ tuone. Na umeme huu, ndiyo usiseme lazima mulume mzima unywee. Ni Bakhresa na wenye nazo pekee anaweza kufurukuta na kusema kata mti panda mti mwenye nazo hakosi walaji. Kama ni apeche alolo what do you do zaidi ya kunywea au kufunika kombe mwanaharamu adunde?

Juzi kwenye ofisi yangu Uwanja wa Fisi nilimsikia mdada mmoja akimpa mumewe, sijui mshirika wake, akisema kama hunazo wenye nazo wala wewe waletewa makombo. Duh! Nilitamani nimnyotoe roho lakini kwa vile cha mtu mavi niliamua kula waya na kuendelea na mihanjo yangu au siyo? Unaweza ukajifanya kukomaa ukamkuta mkeo na kaka yake hasa wale jamaa zangu wa mlima ule. Akionyeshwa njuluku hata dogi anapewa kitu muhimu mnakula sahani moja. Hata hao wanaojiita uncles na kaka chunga sana. Hao hawaaminiki ni sawa na jiko la mchina. Jamani nanyi achene mambo haya mtaishia unung’aembe. Maana mtu aoelewa leo kesho yu ntaaani! Jamani punguzeni kuabudia na kupenda pesa na vitu ni vya kupita. Hata mbuzi hawafanyi hivyo zaidi ya mbwa na kuku.

Kumbe siku hizi kama huna kitu huna bao kama hizi njemba zilizotembezewa ndoa hata kama haramu na kijogoo cha kike! Kama umeingia mkenge na kuoa kwenye mlima ule ndiyo usiseme. Najua wengi wanaosoma walioingia mkenge wanatauna meno na kutikisa vichwa. Shauri yenu kwani mie ndiyo niliwatuma? Je ni wangapi wanafanyiwa hivi na wasifurukute? Nawaambia fanya kama mimi. Timua wapo wengi badala ya kuwa mtumwa wa ndoa. Huna haja ya kujinyong’onyeza na kiumbe asiye na shukrani wakati wapo wengi wanatafuta nafasi yake. Hata wanaume hivyo. Kama nkeo ni mali amelelewa vilivyo ukanchezea jua wapo wengi wanawinda. Hayo tuyaache.

Jamani ee siku hizi wanawake wako aina mbili-mosi vitega uchumi vya wazazi au wale wa ubani. Ukiangukia kwenye akina babangu “kinu lasima kijenge nyumba”, umeumia. Huko mie siko matajuana wenyewe. Kwani wakati mkikubaliana mie mlevi sikuwepo. Nilikuwa zangu Uwanja wa Fisi nikiweka vitu. Hata wanaume wapo akina toto la mother. Wao wanadandia akina dada wenye nazo au nafasi ili wawatumie kupiga pamba na kuishi wasijue ndiyo kuolewa kwenyewe! Hata akina dada wanaoulizwa na mama zao kama wachumba zao ni wafanyabiashara, wanasheria au wahasibu nao hawana maana. Si ujanja. Ni uvivu na umaskini wa kiakili. Kwanini utake mchumba wako awe nazo wakati baba yako hana kitu bali kukutumia wewe kama mtaji? Huu nao ni ufisadi na umalaya. Unamwambia mtu I love you kumbe una-love Pochi lake! Wapo walioambukizwa miwaya wakaacha mipesa nyuma wasiifaidi kutokana na kujiona wao wanjanja wasijue wapo wajanja kuliko wao. This is crazy so to speak. Upendo ndiyo msingi wa ndoa. Zaidi ya hapo ni kupoteza muda. Wewe unataka mie niwe nazo uchume. Je baba yako anazo? Kama unataka mie niwe nazo kwanini wewe usiwe nazo? Huu nao ni uvivu na umaskini. Wenye tabia hizi jamani acheni.

Turejee kwenye ndoa yaani kuolewa na kijogoo cha kike. Kama warume wanaoa, kuna ubaya gani wanamama nao kuoa? Si ndoa ni makubaliano bwana? Ila hapa lazima niweke shurti. Si kila makubaliano si ndoa. Naongopa wale akina saga na senge wasitumie mwanya huu kuhalalisha ufirauni wao. Mbona kuna warume wameolewa na tunawajua lakini hatusemi!

Acha niende kusaka kidumejike kiniwowe haraka mie. Sharti la mwisho kidumejike hiki kiwe waziri au balozi nje.
Chanzo: Dira Agosti 29, 2011.

No comments: