The Chant of Savant

Wednesday 9 November 2011

Je huu si unyanyasaji wa wanyama?



Mswahili akimning'iniza kuku anakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la jinai. Hivi karibuni waziri mhusika alitangaza kuwa atakayewatesa wanyama atafungwa au kutozwa faini kwa maelfu si haba.Ajabu ya maajabu waziri mhusika na serikali yake hakuonyesha kujali kueleza atakachotendwa anayewatesa wanadamu hasa kwa ufisadi na uzembe! Anyway, kuna kipindi wanyama wanakuwa na thamani kuliko binadamu kama mashoga walivyo na haki na thamani kuliko mamilioni ya watu maskini. Turejee kwa wanyama. Picha hiyo hapo juu ni mnyama aina ya kifaru akisafirishwa kwa helkopta umbali wa kilometa 1,500 kama kutoka Dar es salaam hadi DRC tukisie. Zoezi hili lilifanyika huko nchini Afrika kusini. Je kwa kumning'iniza hata kama amekuwa sedated bado si kumnyanyasa? Sina la kusema.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hakika huo ni unyanyasaji mkubwa sana kwa vile hawawezi kusema au? na si unyanyasaji tu ni utesaji pia..

Bennet said...

Sina uhakika na huu umbali, ninachojua kwewnye Vet-medicine hii inaweza kufanyika kwa ndani ya ranchi tu, Mfano huyu kifaru alikuwa anaumwa na inabidi awekwe sehemu kwa muda wa wiki ili aendelee kupata dawa kila siku, basi atapigwa sindano za kumlaza (tanquilizer)kwa njia ya bunduki ndio anabebwa kama hivi