The Chant of Savant

Monday 9 April 2012

Kikwete haishi vituko kama msanii!


Rais Jakaya Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha maombolezo ya Msanii.
Ingawa kitendo cha rais Jakaya Kikwete kukaririwa akisema kuwa aliahirisha ziara ili kumuomboleza na kumzika Stephen Kanumba kinaweza kuonekana ni cha utu, ukweli ni kwamba kinaacha  maswali mengi. Wengi tunajiuliza: Kanumba ni bora kuliko watanzania waliopoteza maisha wakati wa mgomo wa madaktari uliosababishwa na uzembe wa Kikwete?


Je Kikwete amefanya hivyo kwa dhati au kutafuta tukio la kufunika aibu iliyokipata chama chake kushindwa kule Arumeru Mashariki? Je Kikwete ana uchungu na msanii mwenzake kuliko watanzania wenzake? Kikwete alinukuriwa na magazeti akisema, "Nimeguswa na msiba huu, nilikuwa nisafiri lakini nimeamua kuja kuwapa pole ndugu na wasanii wote," Wenye kumbukumbu wanajiuliza: Mbona hakufanya hivyo wakati wa mgomo? Mbona hakuguswa na misiba ya watanzania wakati wa mgomo alipoamua kuwaacha wakilia akaekea zake Davos Uswisi kwenye mkutano ambao hakuwa na umuhimu?


Laiti Kikwete angeahirisha safari yake wakati wa mgomo, angejizolea sifa na heshima kubwa. Maswali yanaendelea.  Je ni kutafuta sifa rahisi rahisi au kutaka kujionyesha kama mpenda watu? Je lipi bora, umahiri wa kuhudhuria mazishi na misiba au kutatua kero za wananchi? Washauri wa Kikwete wanapaswa kurejea darasani kujifunza upya. 

2 comments:

Anonymous said...

Matata kweli kaka yetu sasa ameahilisha safali kwajili ya msiba ulikuwa unataka afanye nini Rais.
What is you point

Jaribu said...

Aendelee na safari yake ya matanuzi?