The Chant of Savant

Tuesday 10 April 2012

Ufilipino: Rais wa zamani mahakamani kwa ufisadi

Image DetailGloria akiwa na mumewe wakati wa siku za furaha.


Rais wa zamani wa Ufilipino Gloria  Macapagal Arroyo alifikishwa mahakamani sambamba na mmewe kwa tuhuma za ufisadi. Arroyo anasemekana kuwa alishiriki ufisadi katika kutoa tenda  kwa kampuni  la mawasiliano ya simu la  Kichina. Mradi husika ulikuwa na thamani ya dola 330. Hii haina tofauti na kinachoendelea nchini Tanzania ambapo huduma za simu zimebinafsishwa kiholela kiasi cha kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye huduma aghali na mbovu za simu barani Afrika. Hata upande wa nishati si salama. Arroyo alitawala Ufilipino kuanzia  2001 hadi 2010. Kwa  habari zaidi BONYEZA HAPA.

No comments: