The Chant of Savant

Wednesday 23 May 2012

Huu mwaka wa Makamba family

Kwa wanaokumbuka tambo za Yusuf Makamba (Mpayukaji) katibu mkuu wa zamani wa CCM kuwa lazima mtoto wake awe waziri, wataamini kuwa Makamba ana hisa kwenye serikali ya Jakaya Kikwete. Ingawa Kikwete aliwahi kukanusha kuwa serikali yake si ya ubia, kitendo cha kumteua junya Januari Makamba kuwa waziri ili kutimiza utabiri wa baba yake ni ushahidi tosha. Makamba family haiishii kwenye siasa tu bali hutumia siasa hadi kwenye uwekezaji ambapo Makamba pia yupo. Binti yake Mwamvita  (pichani)  ssi haba. Ukitaka kujua nimaanishacho, nenda Benki Kuu uone ni watoto wangapi wa vigogo wameajiriwa kule. Kama hiyo haitoshi, angalia orodha ya wakuu wa wilaya wapya uone ni watoto wa vigogo au jamaa zao wangapi wameukwaa. Hiyo ndiyo Tanzania iliyosalia baada ya mafisi na mafisadi kula kitu na kubakisha mifupa na ngozi. Hakika huu ni mwaka wa familia za vigogo ikiwemo ya Makamba.

1 comment:

Anonymous said...

Kwahiyo ile ya kumtoa baba yao kutoka uongozi wa chama ulikuwa geresha tu! Naona sasa wamewekwa watoto wote katika ulaji na baba naye anakula kwa njia nyingine. Inakuwa vipi kumweka mtu au kumpa cheo ambacho hana hata ufahamu wowote. Huyu Kikwete ni "airhead" akili hakuna kabisa.Ni akili ya wizi tu na ni kibaraka kabisa.