The Chant of Savant

Wednesday 9 May 2012

Kulikoni Kikwete na WEF tena?



Kwa wenye kumbukumbu ni kwamba rais Jakaya Kikwete alikuwa nchini Brazil mwezi jana kuhudhuria mkutano wa jukwaa la  kiuchumi wa World Economic Forum. Leo tena tunaambiwa amekwenda kuhudhuria mkutano ule ule ila kanda ya Afrika  kule Ethiopia! Kunani wakati tunajua Tanzania ilivyo zero kwenye uchumi hasa kutokana na utawala kibabaishaji na kifisadi? Je Kikwete atakaa lini ofisini afanye kazi aliyochaguliwa kufanya? Je hii ni haki? Juzi juzi tu ameendelea kuwatwisha mzigo watanzania kwa kutanua baraza lake la mawaziri ukiachia mbali kupenda kusafiri. Je itumike lugha gani lau Kikwete aelewe na kuwajibika? Hapa ndipo saini zaidi za wabunge zinahitajika zaidi na haraka. Kama kawaida yake, ameandamana na nani? Top secet!

No comments: