The Chant of Savant

Wednesday 9 May 2012

Muhingo Rweyemamu:Hatimaye kujipendekeza ukanjanja na ghilba vimelipa

Muhingo Rweyemamu
James Milly alisema kuwa watu wengi kwenye Chama Cha Mapinduzi wanaishi kwa kujikomba na kwa matumaini hasa vijana. Hakuna mtu ambaye amehangaika na kujivua nguo kama Muhingo Rweyemamu ambaye alikuwa tayari kuandika kila sifa na uongo ilmradi amfurahishe Jakaya Kikwete. Kama ilivyokuwa kwa wajina wake Salva Rweyemamu, at last Kikwete amemkumbuka mtwana wake mtiifu Muhingo Rweyemamu mwandishi wa habari aliyejigeuza kanjanja ili atupiwe makombo. Sasa Muhingo si mwandishi wa habari tena bali mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Handeni. Jamani uheshimiwa unaopatikana kwa kujidhalilisha na dharau si uheshimiwa kitu. Hata hivyo Handeni imekula kwao. Kibaraka kama huyu atawafaa nini?

No comments: