The Chant of Savant

Sunday 13 May 2012

Nimetokea kuwapenda hawa jamaa


Stockbyte

Jamaa hawa waitwao Moose wanapatikana sana maeneo ya pwani ya bahari ya Atlantiki nchini Kanada hata baadhi ya sehemu za Marekani kama vile Alaska, Meine, Massachusetts na kwingineko. Ni wanyama wapole kwa kuwaangalia. Ila wanapokuwa na watoto ni hatari sana. Kwani humshuku yeyote awakaribiaye kiasi cha kumtia adabu. Ukienda mitaa ya baadhi ya miji kwenye jimbo la Alaska unakutana nao mitaani kutokana na kuruhusiwa kuwa wakazi wa miji waishimo.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Hapa sweden wapo na wanaitwa wafalme wa msitu...Nyama yake ni tamu nimewahi kula....