The Chant of Savant

Saturday 19 May 2012

Obama amejua kuwatenda akina Kikwete

Kama mwalimu mkuu, rais Obama akimtambulisha rais Kikwete
Tangu vyombo vya habari vitangaze kualikwa kwa rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa viongozi wa nchi tajiri, wengi tulitegemea angalau tatapata picha ya pamoja ya rais na mwenyeji wake Barack Obama wakiwa kwenye maongezi mazito. Sasa picha yenyewe tumeipata ingawa ni kichefuchefu kitupu. Maana picha za kiprotokali zinamuonyesha Kikwete na wanamuziki kama Bono na watu wengine wadogo lakini si Obama. Kinachoonekana kwenye picha hiyo ni casual introduction inayofanywa na Obama kwa watawala ombaomba wa Afrika aliowaalika kuwasanifu. Kazi bado ipo. Iko wapi picha ya rais na rais?

Kikwete akiwa na Bono wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari Shirika la Habari la NBC Andrea Mitchell jijini Washington.

1 comment:

Jaribu said...

"Of course, we want our partners to help us with infrastructure........"
"Of course, we want help with our agriculture.........."
"Of course, I have no idea what I am talking about."