The Chant of Savant

Thursday 17 May 2012

Rais na mcheza mpira wapi na wapi?


  1. Rasi Jakaya Kikwete akiwa na mchezaji mpira wa miguu David Beckham huko London hivi karibuni huku mkewe akishangaashangaa, Wapi mke wa Beckham?
    Ingawa tunaonekana kutomtendea haki, angekuwa anatujibu ukweli ungejulikana. Rais Jakaya Kikwete ameonyesha kupwaya karibu kwa kila analojaribu kufanya. Washauri wake wanamwimbia na kutuibia walipa kodi-wanamkomoa kwa kumshauri vibaya. Tulipoambiwa Kikwete amekaribishwa Marekani kwenye G 8 wengi tuligemea kupata picha akiwa na watu wa maana kama Barack Obama na wengine wazito. Ajabu tunaletewa picha akiwa na wachezaji wa mpira kana kwamba yeye ni waziri wa michezo! Whsat a loss in the first place! Ni pigo kuwa na kiongozi asiyejijua na kujua uzito wa nafasi yake na dhamana aliyobeba.

5 comments:

Anonymous said...

halafu msanii utamjua tuu! basi anapojifanya kumshangaa na kumsikiliza kwa makini huku hakuna kitu.kinapitia sikio la kulia na kutokea la kushoto ila beckham hamjui huyu rais wetu jinsi alivyomsanii

Anonymous said...

Picha imepigwa london mkutano wa g8 upo wapi?

Anonymous said...

Chuki Binafsi zitaisha 2015

Anonymous said...

Picha nyengine hujaziona ?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nimeziona ila nimependa hii kutokana na ujumbe inaotoa kwa wenye akili.