The Chant of Savant

Saturday 26 May 2012

Zanzibar: Huu ni uamsho au uangusho?


Hali visiwani Zanzibar si shwari. Taarifa tulizopata ni kwamba kumekuwa makabiliano baina ya polisi wa kutuliza ghasia FFU na kikundi cha kihuni kinachojiita Kikundi cha Uamsho. Je hawa wanaojiita Kikundi cha Uamsho wanaotaka muungano uvunjwe wametumwa na nani? Je ni yale yale ya kuigiza yale ya wenzao wa Mombasa Republic Council huko Kenya wanaodai kujitenga ili washirikiane vizuri na mabwana zao wa kiarabu? Leo wazanzibari wanakataa muungano wakidai wajitenge wawe huru. Je na Pemba wakidai kujitenga na Zanzibar huru mambo yatakuwaje? Mbona wenzetu wanashindwa kujifunza toka Comoro? Serikali ya muungano inapaswa kuingilia na kuhakikisha kikundi hiki kinashughulikiwa kwa njia stahiki yaani, kuruhusu wananchi kuujadili muungano. Je ni kwanini serikalil ya Muungano imekuwa kimya kwenye tatizo la muungano au ni ile hali ya serikali husika kushindwa karibu katika kila kitu? Je hiki kikundi kinachoanza kutumia mabavu cha Uamsho kinachofanya ni uamsho au Uangusho?

3 comments:

Anonymous said...

naona yamekuchoma ndugu limekuchoma saaana na hata bado huu ni mwanzo tu, ni kawaida ya koloni lilivo, kwa taarifa yako wazanzibari tunachodai ni haki yetu, na tutahakikisha nchi yetu inakuwa huru, ukhanisi basi tena tumechoka, ukoloni wa kitanganyika basiiii tullitawalia na tukapata uhuru, kwa muda mrefu tulidhani nyinyi mngekuwa mstari wa mbele kiudugu kumbe hamnaa maana yoyote,na tunasema na tutaendelea kusema muungano hatuutaki..........., wewe unaumia nini siudai tanganyika yako......... mambo ya znz hayakuhusu maana mtu mzima na na akili zako kuwa na fikra potofu ni ukhanisi, ati wanataka kurudisha mabwana zao wa kiarabu si ndo wewe unaeshadidia chadema mjinga mkubwa wee,au nachadema wanataka kuwarudisha mabwana zao wakijerumani ujinga, mmeshatudhalilisha saana, mpaka raisi wetu mnamfanya waziri ukhanisi gani huu sisi tuchaguwe raisi nyie mumwite waziri ...... tuachiwe tupumuwe

Anonymous said...

Huyu msomi uchwara hana lolote
Zanzibar na pemba ni nchi moja
ikijitenga zanzibar na pemba ipo pamoja hata hajuwi anandika kitu gani

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Tunawashukuruni sana kwa mawazo yenu ingawa hatukubaliani nayo. Kimsingi, binadamu wote hatuwezi kuwa na mwamko na mawazo yanayofanana. Hata katika kusoma ujumbe inaonekana kuna watu hawakuelewa kitu ingawa wamejibu kitu ambacho nacho sicho. Karibuni tena mpatapo fursa acheni nyayo zenu na kutoa dukuduku lenu.