The Chant of Savant

Tuesday 14 August 2012

Meya wa Toronto matatani kwa kuvunja sheria za barabarani



Meya wa jiji la Toronto Rob Ford amejikuta matatani baada ya kugunduliwa akiwa anaendesha gari na anasoma jambo ambalo ni kosa la jinai kwa sheria za Kanada. Ford alikiri kuendesha huku akisoma ingawa alijaribu kujitetea kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi. Hivyo hujikuta ana mrundikano wa kazi. Je angekuwa meya wa jiji la kiafrika angekamatwa? Wenzetu hawana mchezo na sheria na hawajui cheo cha mtu. Miaka minne iliyopita waziri mkuu wa zamani  wa jimbo la New Foundland and Labrador, Danny Willilams alijikuta matatani alipokamatwa na askari mdogo wa usalama barabarani na kutozwa faini pamoja na kuomba msamaha. Ingekuwa Afrika maofisa wa polisi kama hawa waliowakamata wakubwa hawa wangeishia kutimuliwa kazi kama siyo kuonywa kama wangeonewa huruma. Tujifunze na tubadilike kwani madaraka ni mali ya umma na si mali binafsi kama wenzetu wanavyoyatumia vibaya barani Afrika. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: