The Chant of Savant

Sunday 7 October 2012

Kama Bagenda, huyu naye anataka kumtapeli Kikwete?




  1. Tapeli aitwaye Novatus Mutoka na kitabu chake cha "HARAKATI ZA DKT JAKAYA KIKWETE KATIKA KUMUENZI MWL JK NYERERE" mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo ofisini kwake mkoani Dodoma

    Kwa wanaokumbuka kitabu cha hovyo cha "Tumaini Lililorejea" kilichotungwa na Prince Bagenda akijikomba kwa Kikwete ili amkumbuke kama alivyofanya kwa Salva Rweyemamu, wanajua kilichofuatia. Bagenda akiwa msomi lakini mjinga, aliandika kitabu cha sifa za uongo sawa na Julius Nyang'oro ambaye hivi karibuni alikutikana na kashfa ya kughushi.

    Naona sasa amejitokeza tapeli mwingine pichani aitwaye Novatus Mutoka ambaye eti ametunga kitabu cha kueleza Kikwete alivyomuenzi Nyerere! Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi. Kikwete anaweza kumuenzi Nyerere kwa madudu anayofanya? 
    Kumbe hata panya akila ngozi ya simba anamuenzi siyo?Ama kweli wakati umefika wa makaburi ya mitume kufagiliwa na wazinzi na wezi! Kikwete kumuenzi Nyerere ni sawa na Nguruwe kuingia msikitini hasa kama tutaangalia anayotenda.Ama kweli huenda neno kuenzi lina maana tofauti na tunayoifahamu. Huyu kama siyo kichaa basi ni tapeli wa kujifunza. Ingawa si vizuri kuuliza swali lenye kuelekea ku-profile mtu, mbona Mutoka, Bagenda, Nyang'olo wote ni kule kule? Ni wao tu wanaoona mema ya Kikwete au wanajua udhaifu wake wa kutopata muda wa kufikiri? 

3 comments:

Anonymous said...

Blog ya watu63 na hakuna anayesoma na kujibu mwenyewe hajiulizi suala?

Jaribu said...

Nani kakuambia hamna anayesoma? Kujibu siyo lazima kama mwandishi amesema kila kitu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu nakushukuru kwa kumjulisha huyu msomaji wangu anayeonekana kuwa fisadi kunishambulia kila mara. Hata hivyo nina wasi wasi na elimu yake. Maana makala za kiingereza huwa hagusi.