The Chant of Savant

Sunday 14 October 2012

Ukweli vurugu Mbagala si dini bali ujinga na umaskini

         Ukichunguza kilichotokea Mbagala hivi karibuni ambapo makanisa yalichomwa moto na wahuni waliojiita waislam, unagundua kuwa kumbe kilichosababisha vurugu si kitendo cha mtoto kunajisi Korani bali chuki, ujinga, husuda na kukata tamaa. Kilichotokea Mbagala ambapo watoto wajinga wawili walibishania juu nguvu za imani zao kingetokea Masaki wala hakuna ambaye angepoteza muda.

       Hata mahuburi ya kijinga yanayofanywa na watu kama Ponda Issa Ponda huwa hayapenyi Masaki. Mikocheni, Kunduchi na maeneo mengi ya wenye nazo. Hivyo tatizo kubwa tulilokuwa nalo ni kuwa na watu wengi wajinga na maskini waliokata tamaa kiasi cha kuweza kutumia kisingizio chochote kuonyesha hasira zao. Hii huitwa venting kitaalamu ambapo mwenye hasira hutafutia sehemu ya kuzitolea au kuzitapika.

    Wenye kusoma na kufahamu dini watanikosoa. Hata kama hicho kilichotokea kingetokea wakati wa mtume Mohammad asingeamuru upuuzi kama ulioshuhudiwa Mbagala. Nani mara hii kasahau jirani yake Mohammad aliyekuwa akijisaidia njiani mwake ili kumuudhi kila kukicha hadi siku alipoungua akashindwa kufanya hivyo na Mohammad akamwombea na akapona na kusilimu? Tuhitimishe kwa kusema wazi kuwa vurugu za Mbagala zilivikwa udini lakini ukweli ni vurugu za kijinga na kimaskini.

2 comments:

Jaribu said...

Njaa hizo. Hata huyo mtoto mwingine angelipizia kwa kukojolea Biblia asingepata madhara yoyote. Maana kama watu tunataka kuchinjana kwa mkusanyiko wa hayo "makaratasi matakatifu" tuliyoletewa na wageni, the least we can do ni kuyaacha yasimame kwa uwezo wake. Kama hamna aliyegeuka au atageuka kwa mjusi kwa vioja hivyo vya dini zote hizo mbili, tuanze kutafakari kuwa labda tunakosea kuweka msisitizo kwa imani hizo za kale, badala ya kuwa ngangari kwa sayansi na teknolojia.

Anonymous said...

Aliyetoa kuruani yake ikojolewe ana makosa makubwa sana kwani hakunyang'anywa ila alitoa kwa ridhaa yake. Hivyo naye anapaswa kuadhibiwa kwa kukipuuza kitabu kitakatifu cha Mungu. Ila waliochoma makanisa nina wasiwasi na awareness zao pengine kwa makusudi au kiukweli wana uwezo mdogo wa kutambua mambo.