The Chant of Savant

Saturday 19 January 2013

Wafadhili kwa kuchezea akili zetu!

 Hakuna asiyefahamu kukwa taifa la Misri haliwezi kuwepo bila mto Nile ambao hupitia Tanzania na kupata maji mengi toka Ziwa Nyanza. Hivyo, huwa hawapendi tutumie maji ya mto huu hata Ziwa Nyanza kwa umwagiliaji kwa vile tutapunguza kiasi cha maji wanayopata. Kutufumba macho, wamekuwa mstari wa mbele eti kusaidia miradi ya kijima ya kuchimba visima vya maji kwa watanzania ili kutuzuga tusielekeze maji ya mto Nile kwenye maeneo kavu. Kwenye picha waziri wa Maji na Umwagiliaji  Prof. Jumanne Maghembe akikenua wakati wa kukata utepe wa uzinduzi wa visima  30 vilivyofadhiriwa na serikali ya Misri. Kushoto kwake ni waziri wa Umwagiliaji wa Misri Prof. Mohamed Bahaa el-Din Ahmed. Kweli tunapenda sana ufadhili hata kwenye vitu vya kijinga.! Kama mbwa, tunapewa fupa kuruhusu mwizi aibe ng'ombe.

No comments: