The Chant of Savant

Wednesday 6 February 2013

Makinda: Kichaa aliyepewa rungu


Nimetokea kuwa muumini wa Masoud Kipanya. Ingawa yeye anafumba, mie sitafumba. Nionacho hapa ni ule msema wa 'Kichaa kapewa rungu'. Hapa kichaa wetu si mwingine bali Anna Makinda anayedaiwa kusimikwa hapo alipo na mafisadi baada ya spika wa zamani Samuel Sitta kuwaumbua hasa aliporuhusu bunge limchunguze na kumsulubu Edward Lowassa waziri mkuu wa zamani na swahiba na mshirika mkuu wa rais Jakaya Kikwete. Je tutaendelea kuruhusu gari letu la thamani kubwa namna hii liendeshwe na kichaa hadi lini? Je kichaa wetu ataua wangapi kabla ya kuligongesha au kulimalizia gari letu kwenye korongo? Je tungetaka aue wangapi ndipo tustuke? Je kichaa akiuwa watu wakati wenye akili timamu wakiwa mashahidi nani wa kulaumiwa? Maswali ni mengi kuliko majibu.

No comments: