The Chant of Savant

Friday 8 March 2013

Je "ushindi" wa Kenyatta utaiumiza au kuisadia Kenya?



Ingawa matokeo ya uchaguzi uliopita wa Kenya hayajatangazwa, vyombo vya habari vya kimataifa vimeishatupasha kuwa Uhuru Kenyatta amechaguliwa kuwa rais mpya wa Kenya. Anachukua madaraka  miaka 35 baada ya baba yake Marehemu Jomo Kenyatta aliyesifika kwa kusimika mfumo mbovu wa sasa ambapo utajiri wa nchi unafaidiwa na watu wachache.
Uhuru anakuwa rais wa kwanza barani kuingia madarakani huku akiwa anakabiliwa na kesi mbaya sana na mauaji na ukatili dhidi ya ubinadamu mbele ya Mhakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai (ICC) ya The Hague. Pia Uhuru anakuwa rais wa kwanza nchini Kenya kuingia madarakani akiwa tajiri wa kutupwa huku akisifika kumilki maelfu ya heka za ardhi huku wakenya wengi wakiishi kama maskwata kwa kupanga nyumba hata ardhi. Ni rais wa kwanza aliyelelewa ikulu kuchukua madaraka baada ya marais wawili tangu baba yake. Pia anakuwa rais wa kwanza kuwa na makamu wa rais mwenye kukabliwa na mashitaka sawa na yake mbele ya mahakama ile ile. Je hili litaisadia au kuiumiza Kenya vipi? Je nchi za magharibi zinazopigania haki za binadamu zitaufyata na kufunika kombe mwanaharamu apite au zitatoa makucha yake na kuufanya utawala wa UHURUTO kuwa mgumu kiasi cha ima kudondoka wenyewe au kushindwa baada ya miaka mitano?
Lolote lawezekana. Kwa vile  hatujui hekima waliyotumia wakenya kumchagua Uhuru na mwenzie Ruto yetu macho. Kwa vile wenye nchi wameamua kufunga ndoa na watuhumiwa, basi wawe tayari kulipia. Waswahili husema ukipenda ua basi penda na boga. Ila kuna gharama.

No comments: