The Chant of Savant

Thursday 9 May 2013

Angalia wizi na unafiki wa vyama vikongwe Afrika



Kwa wanaomfahamu Julius Malema (32) Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Vijana wa Chama tawala cha African National Congress (ANC) walishangaa waliyosikia baada ya Malema kutofautiana na mwenye chama rais Jacob Zuma. Malema kijana mdogo aliyekimbia umande alikutikana kuwa na utajiri wa kutisha utokanao na tenda za upendeleo na kukwepa kulipa kodi kwa mujibu wa serikali ambayo alifarakana nayo hivi karibuni.

Jengo lisiloisha la ambayo ingekuwa nyumbani kwa Malema (Pichani)


Ikumbukwe Malema ndiye aliyetumiwa na Zuma kumuondoa Thabo Mbeki madarakani akayachukua yeye. Ingawa Malema sasa anaandamwa kiasi cha mali zake nyingi kuuzwa, tunajifunza kitu kimoja kuwa vyama vikongwe vya kizandiki na kidikteta kama CCM vinawatumia vijana wenye uchu wa madaraka na mali na wajinga huku vikiwahonga pesa nyingi. Kama Malema amekutwa na utajiri wa mamilioni ya dola, hao akina Emanuel Nchimbi na Nchemba Mwigulu wana utajiri kiasi gani licha ya kuendelea kupewa vyeo hata kama wanajulikana walivyotenda jinai ya kughushi.
Kinachoshangaza kuhusiana na sakata la Malema ni kuandamwa kwa kesi na kashfa za kujipatia utajiri haraka na kinyume cha sheria wakati mtoto wa Zuma, Duduzane anafanya kile kile kama ilivyo kwa Ridhiwan Kikwete Tanzania. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: