The Chant of Savant

Sunday 12 May 2013

Kwanini Kikwete amejaza taka za kisiasa kwenye balozi zetu?


Kwa wanaokumbuka mstuko uliolipat taifa pale rais Jakaya Kikwete alipowateua watu waliokuwa wameshindwa kwenye chaguzi, nadhani wameshangaa zaidi kusikia uteuzi wa hivi karibuni wa mabalozi wa Tanzania nje. Kikwete alipowateua Didorus Kamala aliyekuwa mbunge wa Nkenge na mtuhumiwa wa kughushi vyeti vya kitaaluma, Dk Batilda Burian aliyebwagwa na Godbless Lema kule Arusha na Philip Marmo aliyebwagwa kule Mbulu, Dk Ladislaus Komba aliyetuhumiwa kwa ufisadi wizarani wengi walipigwa butwaa licha ya kulaani kujuana huku.
Bila kujali hisia za wananchi, kipindi hicho hicho aliwateua watu wa hovyo kama vile Adad Rajab, Jaka Mwambi na Mwanaidi Maajar anayetuhumiwa kufanikisha wizi wa fedha Benki Kuu chini ya skandali ya EPA iliyomwezesha Kikwete kuingia madarakani ukiachia mbali balozi zetu kujaa watoto wa vigogo. 
Hakuna kilichotushangaza kama uteuzi wa Wilson Masilingi kuwa mbunge wa Tanzania Uholanzi. Huyu alibwagwa na profesa Anna Tibaijuka kule Muleba. Huyu sawa na Marmo, Mwambi, Kamala na makapi mengine anaweza kuwa jipya gani kama siyo kulipana fadhila na kujaza makapi kwenye balozi zetu?

2 comments:

Mtwangio said...

Mhango,inapochukuliwa nchi katika muono wa shamba binafsi,nyumba binafsi,kijiji cha ambao kwamba kwa matokeao kam haya wala si ya kuyashangaa si kwa kikwete tu ambaye yupo madarkani kwa wakati huu bali tabia hii imekuwa ni maradhi ya utartibu wa utawala wa nchi yetu.Kwa hiyo sasa kuna umasikini wa kurithi,maradhi ya kurithi,ujinga wa kurithi,elimu ya kurithi,madarka ya kurithi na utajiri wa kurithi.

Serikali yetu kama zilivyo serikali nyingi za afrika tangu katika utwala wa chama kimoja mpaka katika wakati huu wa demokrasia changa bado nyuso za viongozi ambao waliowahi kuingia katika siasa ni zile zile tu hata huwa najiuliza kwani katka siasa hakuna umri wa kustaafu?Na la kushangaza zaidi hata wale waliostaafu jeshini nao wanapewa maulaji ya wakuu wa mikoa na mawilaya na kupelekwa huko kwenye ubalozi.

Je lini serikali yetu itawaheshimu wananchi wao na kuwaona kwamba wao ndio watawala wa kweli?kwa nini viongozi wetu hawana uwoga na nguvu za umma kama zilivyokuwa nchi zingine?wakti wa kupigania ubunge na urais wanakuja kwetu kuropoka,kunafiki na kutufanya kama watoto wadogo kwa kutuahidi ahadi peremende na tunawapa kura zetu kwamba eti mnastahiki kututwala wanapofika bungeni na katika urais tayari wanatuona kama mbwa koko.Na wanajiamini kiasi gani viongozi wetu hawa bila ya kusoma alama za nyakati kuanzia,Tunisia,Egypt,Yemeni,Libya na domino imeshaangukia Syria.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mtwangio amini usiamini kuna siku watabadilika. Naamini hivyo kutokana na jinsitunavyowatumia ujumbe. Kama utakumbuka miaka iliyopita hapakuwa na nyenzo kama hizi za kuwafikishia taarifa. Hata kama tunaojitoa mhanga kuwaambia wasivyotaka kusikia ni tone katika bahari, wahusika wanapata salamu vizuri na kuzifanyia kazi. Mfano mdogo, mke wa Kikwete alipokuwa akitumia anwani ya ikulu kwenye biashara yake ya WAMA, niliandika kulaani kitu hiki na kuwatumia nakala. Baada ya siku mbili wavuti wao uliondoa hiyo anwani na kuzuia mawasiliano kwa email au njia yoyote. Ukitaka kujua hili pekua wavuti wa wama halafu uchukue zile emails zilizoandikwa pale utume ujumbe hautakwenda. Hivyo sina shaka kuna siku wataelewa au kubadilishwa kwa vile siku hazigandi.