The Chant of Savant

Saturday 18 May 2013

Nilipata zawadi ya ubongo juzi



Licha ya kuwa mtunzi, nina mapenzi makubwa na vitabu nina mapenzi na heshima kubwa kwa watunzi. Juzi nilipata zawadi ya kitabu cha 'The Constructed Mennonite' toka kwa mtunzi (Author) ambaye ametokea kuwa rafiki na mentor. Huyu si mwingine bali Profesa Hans Werner ambaye ni mwalimu na nguli wa historia ya dini ya Kimennonite. Ingawa hili si eneo langu la kujidai, huwa najisomea historia hii kwa muda wa ziada ili kuona ni kiasi gani jamaa hawa walipatilizwa na utawala wa kanisa la Kirumi la Kikatoliki kwenye karne ya 18.
Hiki ni kitabu cha tatu toka kwa mwandishi kikiwa na saini yake. Kitabu cha kwanza 
nilipata cha The 'Z-Z of the Great Britain' toka kwa mwandishi Dixe Wills wa London ambaye naye ni rafiki yangu na cha pili cha 'Endless Toil' toka kwa Attilio Tagalile wa Dar es salaam ambaye pia ni rafiki yangu. Kwa mtunzi ni furaha ya aina yake kupata nakala ya kitabu ikiwa imesainiwa na mtunzi mwenyewe.Ni sawa na kuwa wa kwanza kukipakata kichanga toka kwa mzazi.

No comments: