The Chant of Savant

Monday 6 May 2013

Wanachopaswa kujifunza CHADEMA toka kwa Profesa Baregu


Habari kuwa profesa Mwesiga Baregu amekigeuka chama chake hadi kupongezwa na CCM (BONYEZA HAPA) si za kufurahisha ukiachia mbali kumuonyesha kama mchumia tumbo na msomi ambaye hakuelimika. Inashangaza msomi kama Baregu anashindwa kufahamu kuwa alitumwa kwenda kwenye tume ya katiba kama mjumbe wa CHADEMA na si kama Baregu. Hivyo, alipaswa kuelewa kuwa wakati wowote waliomtuma wanapoamua kumrejesha awe amekosea au la ni haki yao. Kwani anachofanya ni dhamana toka chamani.
Hata hivyo, tunaojua elimu ya Baregu yaani kile alichosomea na kufundisha tulishangaa kumteua mtu asiyejua sheria wakati kulikuwa na magwiji wa sheria kama Profesa  Abdallah Safari. Kwa vile Baregu ameishakuwa mbuzi badala ya mbwamwitu, umefika wakati wa CHADEMA kumlazimisha aachane na kulazimisha kuwa mjumbe wake. Kama motisha wa kutaka kuendelea kufanya kazi ambayo hakutumwa wala kuwaridhisha waliomtuma ajiunge CCM aendelee kulipwa hizo laki tatu kwa siku kama kaona ni dili.
Somo ambalo CHADEMA wanapaswa kujifunza toka kwenye kadhia hii ni kuwa makini wanapoteua watu wa kuwakilisha chama. Pia wajaribu kuteua watu wenye taaluma na jambo husika badala ya kuangalia ukongwe au mambo mengine. Tumalizie kwa kusema kuwa alichofanya Baregu ni aibu, uroho, roho mbaya, uchoyo na uchumiatumbo.

No comments: