The Chant of Savant

Thursday 11 July 2013

Kikwete ateua fisadi mwingine kama ishara ya kulindana

Rais Kikwete akimwapisha Hilda Gondwe kuwa mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikulu Dar.Kikwete katika picha ya kumbukumbu na Gondwe Ikulu.

Uteuzi wa Hilda Gondwe aliyekuwa Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro ni ushahidi wa rais Jakaya Kikwete kulinda mafisadi.  Mnamo tarehe 27 Mei 2010 blogu hii ilchapisha kashfa iliyomkabili Gondwe ambao alijitwalia gari la umma aina ya Toyota Land Cruiser VX iliyokuwa imenunuliwa miaka mitatu kabla kwa shilingi 155,000,000. Gondwe 'alinunua' gari hili kwa shilingi milioni moja na nusu tu huku akiusababishia umma hasara ya shilingi 149,000,000. Je rais na washauri wake hawakuliona au hawalikumbuki hili? Je inatoa picha gani kwa umma wa walipa kodi maskini wa nchi yetu? Ni ajabu kugundua kuwa mtu huyu ameteuliwa na rais kuwa mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Viongozi wa umma nchini. Je anaingia mtu huyu asiye na maadili mle na maadili gani zaidi ya madili? Je huu si ushahidi mwingine wa Kikwete kulinda uoza na kutokuwa makini na kurudia makosa? Je hakuna watanzania safi wenye kuweza kufanya kazi hii hadi wateuliwa wahalifu wa kawaida kama Gondwe? Je Kikwete atajifunza na kubadilika lini? Je kuna haja ya umma kuendelea kumvumilia mtu kilaza kama huyu  mgumu wa kujifunza na kubadilika? Hakika, maswali ni mengi kuliko majibu.

2 comments:

Jaribu said...

Kikwete anawapenda hao wasiokuwa na maadili. Wanamsadia kutuibia!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ila ipo siku watarejesha hicho wanachokwapua kwa kupeana fadhili. Mungu awalaani na walaanike na mapema. AAAAAMIN.