The Chant of Savant

Saturday 22 February 2014

Ukraine: Nguvu ya umma yamng'oa rais

... Tymoshenko – Letter to Ukranian President Viktor Yanukovych | News
Sasa si gumzo wala majungu. Viktor Yanukovych's aliyekuwa rais wa Ukraine ameangushwa na umma. Hii ni baada ya kukumbwa na maandamano ya zaidi ya miezi mitatu. Yanukovych alipatwa na yaliyomkuta baada ya kupinga juhudi za Ukraine kujiunga na jumuia ya Ulaya (EU). Pamoja na msimamo wake mkali akiungwa mkono na Urusi, Yanukovych alijikuta akipinguduliwa kutokana na mapigo mawili moja likiwa ni bunge kupiga kura ya kumuondoa madarakani na pili waandamanaji kuendelea kukaa mitaani pamoja na baridi kali kwa zaidi ya miezi mitatu. Msumari wa mwisho kwenye geneza la Yanukovych kisiasa ulipigwa baada ya kuachiwa kwa hasimu wake mkuu waziri mkuu wa zamani Yulia Tymoshenko aliyewashukuru wananachi kwa kuleta mabadiliko na kuomba wasiondoke mitaani hadi kieleweke zaidi.

5 comments:

Anonymous said...

Kujitambua kunaendana kujifunza & kufindishwa kutoka katika elimu shindani na maarifa yanayojenga mhtimu jinsi ya kupambana na changamoto katika mazingira katika mahala ulipo....

Sasa kwa watanzani inakuwa ndoto sababu tumekosa hili suala nililolitaja hapo juu ni kikwazo kikubwa sana ndugu yetu Mwalimu NN Mhango.

Angalia hata matokeo ya kidato cha nne yanaingiliwa na utaratibu unayopunguza uwezo wa wahitimu kupamba na mazingira yao wahitimu....!

Jaribu said...

Ni kweli Anonymous, wakoloni walikuwa na "Divide and rule", vihiyo wetu wa CCM wamekuja na, "Dumb down and rule."

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon na Jaribu hamjakosea. Mara nyingi huwa ninaamini kuwa tunatawaliwa na wakoloni ambao wakati mwingine ni wabaya kuliko weupe hasa ikizingatiwa kuwa hawana uchungu nasi wakati ni ndugu zetu. Mfano mdogo ni suala la ujangili. Wakoloni walikuja wakatumia wanyama wetu lakini wakatubakizia. Uliza hawa majangili wa kisiaa wa sasa wanafanya nini. Wanataka wakiondoka na wanyama watoweke. Tuna deni moja kubwa kwetu binafsi na taifa letu ambalo ni kujitambua ili tujikomboe.

Anonymous said...

Mhango, hii safari ndefu sana ya kujitambua maana ujinga na mambo ya hatari ndiyo yanashabikiwa na hao wanaotaka kushika dhamana ya uongozi..!

Hivi karibuni kuna mtu mmoja aliyesema ana ndoto na watanzania, alikwenda kwa wanaoitwa bodaboda na kusifia kwamba wamengeneza ajira kwa vijana.....!

Moja, Hivi kuagiza piki piki nje ya nchi ni kukuza uchumi au kuamisha uchumi?

Pili kunatakwimu zozozte za tafiti kamili za kisayansi zilizotolewa mpaka kuhusiana na bodaboda kwamba ni watu wangapi wamepata ulemavu wa viungo au kupoteza maisha, na gharma serikali ilizoingia kutokana na matukio hayo.

Tatu Je haoa abiria wa Bodaboda wanapopata ajali kuna bima yoyote inayolinda maslhai ya abiria baada ya ajali?

Nne Serikali hapo imehamisha tuu tatizo kwa kulipaka rangi nyingine ingawa msingi tatizo kutowekea mkazo kwa dhati katika kilimo ambacho Tafia ndiyo msingi mkuu wa mapato yake na usalama wa uchumi wetu....

Asante Mhango

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon
Kama sikosei huyu ni EL Ewassa mmeru anayejiita mmasai. Nijuavyo ni kwamba hii biashara kama aliisifia jua alikuwa akiwaingiza mkenge ili yeye mkewe mwanae au mshirika wake aagize hizo pikipiki na kuwalangua na kutengeneza fedha akiwaachia balaa la kufa katika ajali bila bima wala maandalizi. Nchi yetu sasa inaendeshwa na wasanii wa kila aina.
Natofautiana nawe hasa unaposema kilimo ndiyo msingi mkuu wa mapato. Bila kuboresha kilimo tukaendelea kutegemea jembe la mkono yatakuwa yale yale.