The Chant of Savant

Saturday 22 March 2014

Mabilioni ya Uswizi: Mlevi achonga na Wereeema



Si kawaida ya mlevi kuandika barua hasa kwa watu wanaojiona au kuonekana mashuhuri. Leo huu mwiko nauvunja.
Ni kutokana na uchugu wa kusoma habari ambazo zinakaribia kuninyotoa roho. Japo huwa najitahidi kukwepa mifadhaiko na ‘frustrations’, hili la kuzidi kuibiwa njuluku za walevi limenishinda. Nimekunywa sana ili kuondoa mawazo.
Nimevuta sana mibangi kama kawa lau nijihisi niko majuu kama siyo Dodoma bungeni.
Lakini wapi! Jinamizi la habari kuwa njuluku zilizokwapuliwa na kufichwa Uswazi ya Uswizi linazidi kuniandama.
Najikuta nimekonda ghafla bin vuu utadhani ninaumwa miwaya.
Hivyo, leo naamua kumtokea jaji Freddie Wereeema aliyetuahidi kuwa njuluku zetu zingerejeshwa toka Uswizi lau zitumike Uswazi.Nianze kwa kumuamukua mura Wereeema.
Mura mbuya? Unaendeleaje na uchunguzi wa njuluku zilizofichwa Uswizi? Juzi nimesikia kuwa walioiba njuluku zetu wanazihamishia Dubei. Je! ni kweli au umbea wa vyombo vya habari?
Mura, naomba ufahamu wazi, kama kweli hizi njuluku zimehamishwa na huna mpango wa kuzirejesha, jua utanikosa. 

Na kama utanikosa baada ya kujinyotoa roho, sina shaka Maulana atakupiga laana unyotoke roho ghafla kwa shinikizo linalonishinikiza kuandika na kuvuta na kunywa kama sina akili nzuri.
Mura, una habari kuwa walevi wengi wanapukutika kwa magojwa yanayotibika kutokana na kuwa apeche alolo, kukabiliwa na ukapa na hata ukiwete? Je! hiyo njuluku tunayoambiwa ni mabilioni ingeokoa walevi wangapi? Walevi wamepigika hadi wengine kukimbiwa na wake zao ukiachia mbali wanaonyanyaswa kila siku kutokana na kutoweza kulisha vitegemezi vyao.
Haya yakitokea, wajivuni waso haya tena vibaka na matapeli wanapayuka na kutapika wakisema kuwa njuluku bilioni 120 ni vijisenti vya ugoro.
Ajabu wakati wakikufuru hivi, nyinyi mnaendelea na politiki kana kwamba mchezo wenu hauna madhara kwa walevi. Mchezo wenu ni mauti yetu ndugu yangu.
Mura, unakumbuka kuwa uliwahi kusema kuna uchunguzi uliokuwa ukifanyika kuhakikisha njuluku zetu zinarejeshwa?
Uliposema hivyo mimi nilikuamini ingawa walevi walionyesha shaka hasa ulipomtisha balozi wa Uswizi huku Uswazi ya akina ombaomba na toboatoboa ukiachia mbali kopakopa.

Ulimwambia kuwa hakupaswa kueleza ukweli kuwa wao walitaka kuwasaidia kurejesha njuluku lakini kwa vile walioficha zile njuluku kule ni wenzenu basi uliamua kula pini na kutoa vitisho.
Mura, unapaswa kufahamu na kukumbuka kuwa watasha si kama nyinyi. Ukiiba hata ufiche kwao watakuwasha tu bila kujali kama utachukia au kujinyotoa roho.
Hivi ninavyoandika, napanga kwenda kuonana na huyo mrume aitwaye Olivieer Chavie ili anipe data nami niwawashe bila huruma.
Kuna kipindi napanga hata kwenda Afghanistan lau nijifunze kujilipua ili nije na kuwalipua hawa mibaka wanaobaka uchumi wetu. 
Naapa haki ya mama na bibi babu na babu wa bibi wa shangazi wa bibi wa bibi wa bibi yangu kuwa nitaondoka na mtu mie.
Na hakika sitanii. Inauma kuona ninavyoendelea kupondwa na dhiki huku mkiponda raha tena kwa njuluku za walevi.
Mura, una habari nilikuwa nakuamini kuliko hata huyo aliyekuumba anayejulikana kwa kuwa bingwa wa sanaa na dana dana?
Tangu alipogwaya kuwasulubu wauza bwimbwi, majambazi na mafisadi imani yangu kwake ilitoweka na kupotea kama ile ndege ya Malaya iliyopotea hivi karibuni bila kuacha hata chembe ya ushahidi. Sina imani na kiumbe huyu. Ninachofanya naomba kila uchao amalize ngwe yake na akitoea angalau nipumue.
Naomba kila uchao aje mrume mwenye udhu na uthubutu ili nimpe ushauri kuwa aende China atuletee majaji wa kweli wa kuhukumu wezi, majambazi, mafisadi na hata majangili bila kusahau wauza bwimbwi na wauza maneno majukwaani wanaotumia siasa kutumaliza.
Mura, haki ya Mungu usikie. Hapa ninapoandika, walevi wana maya na wezi ajuaye ni Subhana mwenyewe. Kuna siku walitaka wachukue michupa yao na kuingia maofisini na mitaa ya Uzitoni na Ugabacholini kuwapiga nayo wale wanaojua kuwa wanatula sisi na mali, madini, wanyama, nyara na fweza zetu.
Mura, najua fika kuwa mmezoea kutuchukulia kama hamnazo kwa vile tu walevi.
Hivyo, hamna hofu kuwa tunaweza kuwageuzia kibao. Kuna kipindi natamani nihamie Libya lau kujifunza wale jamaa walivyomnyotoa roho mjivuni Mwamari Kashafi aliyenyotolewa roho akilia kama kibaka. Siku hiyo nilikunywa na kuvuta kama sina akili nzuri.
Na hao wanaoiba njuluku zetu na kuzificha Uswizi na baadaye kuzihamishia Dubei natamani nishuhudie kiama chao tena majilini kwenye mikono ya walevi wakiwachoma moto kama vibaka.
Mura, hivi ni kweli au umbea wa waandika maneno? Hakuna kitu kiliniumiza kama kusoma nukuu hii, “Hili jambo ni jambo nyeti sana kwa sababu kazi tuliyopewa kuchunguza suala hili bado hatujamaliza, kwa hiyo kuanza kulizungumza kwenye vyombo vya habari kunaweza kuathiri kazi hii.”
Je! ni kweli ulisema hivyo? Je! uchuguzi wenu ulikuwa ni wa kutafuta mahali pa kuhamishia au kuwazuga walevi?
Maana haiingii akilini kwa mtu anayesaka mwizi na mali alizoibiwa akaambiwa zilipofichwa na zinakohamishiwa akajifanya hamnazo kwa kusingizia sijui uchuguzi sijui unyeti na mambo kama hayo.
Huu nao ni ufisadi wa kiakili ambao wagiriyama huita ‘intellectual corruption’. ‘Yes, this is damn mental slavery geared by greed and myopia’. ‘Do you think we are all goons and zombies to bless such sacrilege?’
Oh samahani! Nimechukia hadi naongea kigiriyama bila sababu ya msingi.Mura, nasikia wewe ukiitwa pilato mkubwa. Je! wewe ni pilato kweli au Yuda?
Nasikia kuwa kuna mapilato kwenye kaya wanasifika kutoa hukumu za kuwapendelea mafisi na mafisadi na wezi wa njuluku za walevi.
Mmoja wapo anaitwa Joni Utumwa aliyeweza kugeuza ‘bedroom yake extra debito judiciae’ yaani chemichemi ya haki.
Wapo wengi wanaowaachia wauza bwibwi ambao siku moja nitawataja.
Leo sisemi mengi zaidi ya kukusihi wahusika waache ‘monkey business’ warejeshe njuluku zetu kabla sijajinyotoa roho kwa kujilipua mibomu. Na hakika sitanii zamu hii. ‘Be warned’

Chanzo: Nipashe Machi 22, 2014.

8 comments:

Jaribu said...

Huyo nilimdharau toka aliposema kuwa Dowans lazima walipwe, halafu haoni hata aibu kujiiita jaji. Jaji my foot!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu hujakosea. Huyu ni junk si jaji. Hana tofauti na Chenge aka mzee wa vijisenti tofauti ni kwamba wizi wake haujafichuka.

Anonymous said...

Zipo Dubai na safari haziishi Kila wakisafiri lazima wapitie Dubai. Kuna Watu wao huko

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon
Mwageni news ili wajue kuwa tunajua walikozihamishia njuluku zetu. Natamani tupate ithibati na uthubutu tuwawachome moto kama vibaka maana wao ni mibaka.

Jaribu said...

Nashangaa kwa nini Waswahili wanawavumilia hawa wakati mwizi wa chupi watamkimbiza mji mzima na kumshughulikia. Hawa wezi wa 'pesa za ugoro' ndi wanafaa wavishwe tairi la moto.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu usishangae ndugu yangu. Tatizo ni ibada za sanamu na vitu kwa waswahili. Hebu angalia wanavyoabudia wahindi wezi na wenye roho mbaya wakati wao wanatuchukia kwa rangi yetu lakini hatuwalipi jino kwa jino. Tazama jamaa zetu waarabu walivyokuja wakatupelekea utumwani wakituuza kwa wazungu halafu wakarudi wakaendelea kuoa dada zetu wakati wao hadi leo wanawakimbizia mabinti zao ima arabuni au kuozeshana kaka na dada kutuepuka na bado hatupati somo. Tusipobadilika kuna siku tutajikuta tukiuzwa utumwani tena.

Jaribu said...

Namkumbuka mpuuzi mmoja alivyokuwa anawatetea Wahindi eti kwa kuwa serikali ya India inatoa scholarship. Shida ya Waswahili dhiki ni umbumbumbu umesaambaa ndio maana sikushangaa sana kumuona Mtanzania padri wa kanisa la kigiriki au muumini wa Ahmaddiya. Of course kila mtu ana uhuru wa kuamini anachotaka lakini wakati mwingine mimi naona hatuna priority na vitu tunavyoshabikia.

Ilibidi nimpe vipande Mzanzibari mmoja aliyekuwa anatamba kuwa Waswahili hatujastaarabika kwa kuwa yeye sijui bibi yake alibakwa na Mwarabu au something. Ilibidi nimwambie just because wewe ni product ya inbreeding haikufanyi wewe ni bora kuliko mtu wa bara. Sipendi kuwasakama watu kwa hili jambo lakini wakati mwingine unachoka.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu,Huyo mzanzibari ungetaka kummaliza ungemwambia aende huko uarabuni wanakodai ni kwao aone anavyobaguliwa. Hili ni tatizo linalowasumbua wasudan wengi wanaojiita waarabu. Wakienda nchi jirani pale Misri wanaitwa chokolate au abid yaani watumwa. Ni upuuzi kwa watu kama hawa wasiojitambua. Nilikutana na wasudan hapa Kanada eti wanakaniambia kuwa mimi ni mwarabu. Niliwajibu kuwa tusi la mwisho ninaloweza kuvumilia ni hilo. Kwa ufupi ni kwamba wahindi wanakimbia umaskini kwao kama sisi tunavyoukimbia kwetu kuja huku. Ukilinganisha kiwango cha umaskini india na Tanzania sisi bado tuna nafuu hata kama hatuambiwi kuwa ni moja ya chumi kubwa duniani. Tatizo la watu wetu ni kutotaka kujitafutia maarifa na kujikubali. Ndiyo maana utakuta watu kama wapemba wanajiona waarabu na waliostaarabika wakati ni wana haramu weusi mbele ya waarabu. Imefikia mahali hata wazaramo wa kutoka Kigoma nao wanawaona watu wa bara kuwa hawajastaarabika. Hapa hujaenda kwa waislamu na tusi lao la kipumbavu la makafiri.