The Chant of Savant

Saturday 24 May 2014

Zuma: Mkombozi au mroho tu wa kawaida


Hapa chini ni makazi ya kifahari ya rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye ameapishwa leo kwa kipindi kingine cha pili na cha mwisho kama rais. Ameahidi mengi kubwa ni kuboresha maisha ya wananchi wa Afrika Kusini. Kujua kama kweli Zuma anamaanisha anachosema, tumeweka hiyo picha ya makazi yake ya kifahari yaliyozamisha mamilioni ya rand huku jirani yake kukiwa na  kibanda cha wale anaosema ataboresha maisha yao. Je kama alishindwa kufanya hivyo miaka mitano iliyopita ataweza kwenye kipindi hiki cha lala salama?Je ni yale yale ya Maisha Bora kwa Wote wote waliolengwa wakiwa ni familia na marafiki na waramba viatu wa rais? Hakika yetu macho kungoja kuona Zuma atakavyowakomboa au kuendelea kuwanyonya na kuwazamisha wananchi.

2 comments:

Anonymous said...

Tatizo kuu la matatizo na changamoto katika Bara la Afrika siyo suala la jinsi ya kutawanya rasmali tuu bali ni uelewa wa maana ya kura na kupiga ni nini gharama zake kwa wapiga kura. Wapiga kura wote Afrika wategemea madiliko katika maisha yao pasipokujua umuhuhimu na thamani kura zao katika kuhadhibu viongozi wabadhirifu, wezi, majambazi, mafisadi, majangili, maharamia na wakandamizajia wa haki na uhuru wa kujieleza.

Tunaishi kwa kutegemea miujiza wakti maendeleo hayahitaji miuijiza...tunatakiwa kujitambua, kujifunza mambo mapya ya maendeleo kuwa wabunifu na pia kukubali kukosoloewa ili kupamabana na changamoto zinazotuzungukua katika maisha yetu ya kila siku.

Angalia viongozi karibuni wote waafrika wanapougua au kuanglia afya zao wanalazimika kwenda nchi nje ya bara la Afrika kupata matibabu. Hii hiyo inaoanesha jinsi gani hatunna wivu wa maendeleo. N a hakuna wananchi waliowahi kuliona ili kama tatizo kugoma nchi zima iwapo likitokea.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon hapo juu hakika umemaliza yote. Hata hivyo, tunahitaji kuwaelimishwa wapiga kura wetu lau wajue wanachotengeza kwa mikono yao.