The Chant of Savant

Tuesday 19 August 2014

Makinda anapodhihirisha ubovu wake

        Japo Tanzania haina utamaduni wa kuwajibika, kuwajibishana, tokana na umma kuwafumbia macho wanaopaswa kufanya hivyo, kuna haja ya kubadilika. Ni wakati muafaka sasa kwa umma wa watanzania ambao, kimsingi, ndiyo waathirika  wakubwa wa ufisadi na wizi unaoendelea katika ofisi za umma kuanza kubadilika ili kubadili jamii kwa ujumla na kuondokana na ubovu huu.
Leo tutaongelea baadhi ya mawaziri na maafisa wengine wa juu wanaokabiliwa na tuhuma za wazi ima za wizi wa fedha za umma au matumizi mabaya ya vyeo vyao. Hawa, kama Tanzania ingekuwa na utamaduni wa kuwajibika kama sehemu ya uongozi bora, walipaswa kuwa nje ya ofisi wanazokalia na kuendelea kuzitumia vibaya.Tutaongelea mawaziri Anna Tibaijuka (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi), Sospiter Muhongo (Nishati na Madini),  na Katibu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, Saada Mkuya (Fedha na Uchumi), Mwanasheria mkuu wa serikali Fredrick Werema na Gavana wa Benki kuu Benno Ndulu, Maafisa tajwa wanatuhumiwa kwa makosa mbali mbali kuanzia wizi wa fedha za umma hadi matumizi mabaya ya ofisi za umma. Kwa mfano, mawaziri Muhongo, Katibu wake Maswi na Ndullu wanakabiliwa na tuhuma za kuchota pesa ya umma bilioni 200 toka kweye akaunti ya ESCROW. Hii si pesa ya ugoro wala vijisenti. Ni pesa ambayo kama ingetumika vilivyo ingeweza kuleta nafuu kwa watanzania maskini wa kutupwa. Ajabu ya maajabu, hata baada ya kushutumiwa na wabunge, wahusika wameendelea kukaa ofisini huku wakitoa visingizio mbali mbali kana kwamba hawahusiki na kashfa husika. Hata kama hawajapatikana na hatia, wangekuwa safi basi wangejiwajibisha kwa kuachia ngazi ili ukweli ujulikane na kuwaweka huru. Kama alivyowashauri mbunge mmoja, kama wana hakika hawahusiki na wizi husika, wangoma nini kuwajibika? Ni bahati mbaya hata aliyewateua anajulikana kwa tabia yake ya kukingia kifua wahalifu.
Waziri Tibaijuka, sawa na wenzake, ametuhumiwa na wabunge kwa ufisadi mkubwa kwenye sekta ya ardhi. Badala ya kuonyesha usafi, udhu, ukomavu na uwajibikaji, naye anaendelea kung’ang’ania ofisi huku akitafuta wachawi na kutoa visingizio vya kitoto. Wajibikeni. Inashangaza kuona wahusika ambao wengi ni wasomi kufanya mambo kana kwamba hawakwenda shule. Muhongo na Tibaijuka ni maprofesa wanaopaswa kuona mambo kwa uoni mpana kuliko watu wa kawaida. Ukiangalia wanayotenda na jinsi wanavyoyatenda, unapata wasi wasi na usomi wao. Dhana hii inazidi kupata nguvu hasa ikizingatiwa kuwa mawaziri wengi tu wanaojulikana kwa kughushi wamo kwenye baraza la mawaziri. Inakuwa vigumu kutofautisha walioghushi na ambao hawakughushi kwa mawaziri hawa hasa ukiangalia utendaji wao na majibu wanayotoa dhidi ya kashfa zinazowakabili.
Mawaziri hawa wanatukumbusha kisa cha mwenzao ambaye naye anaokena kuwa msomi Dk Shukuru Kawambwa ambaye licha ya kuua elimu yetu, ameendelea kujifanya hayamhusu hata alipotakiwa aachie ngazi ili wenye uwezo na uchungu wachukue nafasi yake. Ni jambo la aibu kwa rais na mawaziri wake kushindwa kujua kuwa uwajbikaji ni msingi wa utawala bora na wa sheria.
Kuhusiana na tuhuma za wizi dhidi ya Muhongo, Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila alikuwa na haya ya kusema, “Mheshimiwa Spika, hakuna dhambi mbaya duniani kama unafiki. Kama kweli Bunge hili linataka kujua ukweli, tuunde Kamati Teule, watu wametoa bilioni 200 kumpa Singasinga ambaye kule Kenya alikumbwa na skandal ya Goldenberg iliyoiangusha Serikali ya Kenya.“Ushahidi ninao, lakini kila nikitaka kuuleta spika anakatakata kona.” Je ni kwanini spika anapiga chenga? Je huu si ushahidi mwingine kuwa spika wa Bunge Anna Makinda alisimikwa hapo kuwalinda mafisadi kama ilivyodaiwa wakati wa kumuengua Spika wa zamani Samuel Sitta? Je Spika anakataa kuunda kamati ya kuchunguza kashfa hii kwa sababu zipi? Kuna haja ya kumwambia Spika kuwa bunge si mali yake au ya chama chake bali mali ya watanzania wanaoibiwa huku akiwalinda wezi wazi wazi. Naye anapaswa kuwajibishwa  kwa vile hafai na si kwa hili tu bali kwa mengi tangu asimikwe kwenye kiti cha spika.
Kashfa nyingine ziko wazi wala hazihitaji hata kufanya uchungzi. Kashfa hizi mbili ya ardhi na wizi wa ESCROW ziko wazi. Tibaijuka ametajiwa kiasi cha ardhi alichokwapua na kilipo wazi wazi. Hakupinga. Badala yake aliingiza siasa kwenye shutuma ili zionekane ni za kisiasa sambamba na Muhongo ambaye amedandia maadui zake kuwa ndiyo wanaomchafua badala ya kupangua hoja kwa hoja zinazoingia akilini. Viongozi wasiopenda kuwajibika, licha ya kuwa waroho na wenye roho mbaya, ni wahalifu wa kawaida wanaopaswa kuwa mbele ya mahakama. Je watanzania wataendelea na woga na uvumilivu huu ambapo sasa umefikia kiwango cha ukondoo hadi lini? Kila ajae anajiibia atakavyo. Imefikia mahali nchi yetu inaonekana kama inakaliwa na raia hamnazo kwa jinsi tunavyotenzwa.
Je hii pesa ya ESCROW, kwa mfano, imeibiwa na maafisa tajwa pekee au kuna mkono mkubwa zaidi ya huu hasa ikizingatiwa kuwa kila unapokaribia uchaguzi hutengenezwa mazingira ya kuiba pesa ya umma ili kutumika kwenye hongo kama ilivyotokea kwenye ujambazi wa karne wa EPA unaosemekena kumsaidia rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani na asikanushe. Je wahusika wanakataa kuwajibika kwa vile wanajua kuna wakubwa wao walioshirikiana nao kuiba fedha husika?
Kitendo cha Spika kukwepa kuunda kamati teule ya bunge kuchunguza ujambazi huu kinaweza kutumbua macho kuwa wezi ni wengi zaidi ya hawa tuliotajiwa na Kafulila. Tutumie fursa hii kumshauri Kafulila aendelee kuwaumbua wezi hawa hadi kieleweke.
Wakati wa kuwawajibisha Makinda, Maswi, Muhongo na Ndullu umewadia. Watanzania tukatae kugeuzwa asusa huku tukiendelea kuambiwa haya ndiyo maisha bora kwa wote. Tuukatae ukondoo na utaahira wa kujitakia ambao unatumiwa na kila vibaka na majambazi wa kalamu kutuangamiza kama jamii na taifa.
Chanzo:Dira 

5 comments:

Anonymous said...

Huyu nungaembe hana lolote bali kuuza sura. Tunajua alipendekezwa na mafisadi ambao sasa anawalinda kwa udi na uvumba. Nasikia eti wanampendekeza awe rais. Yaani balaa jingine baada Jakaya!

Anonymous said...

ANA NINI HUYU ANA TANGU ALIPOKUWA SPIKA ANASEMA JINA LAKE ANNE
JAMANI HILI SAGO LA KUTUPWA KWA NINI HANA MUME WALA MTOTO CHAKULA CHA CCM TANGU AWAMU WA KWANZA

Anonymous said...

ANA SURA GANI KUVAA MAWIGI NA MKOROGO

Anonymous said...

TANGU AMEKUWA SPIKA ANA MDOMO NA VYODO ANASEMA ITI SASA HAMUWEZI TUNAWEZA SANA 2015 ANNNNNNNNNNNNNNNNNNNNNNNAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA NOT ANEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE BI MAKINDA MSAGO UNAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA LAKO

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon wote hapo juu mmesikika. Kazi kwa wahusika kutilia maanani ukweli kuwa mmeishastuka na hamko tayari kuchezewa shere. Nawashukuruni kwa michango yenu.