The Chant of Savant

Sunday 30 November 2014

Picha ya mwezi toka Missouri

Imekaaje hii ya Chenge na mkokoteni wa minoti?


Kikwete azidi kuwatoa kafara wenzake akiendelea kutesa



Uamuzi wa Bunge kuwashughulikia mawaziri na wabunge wachache ni pigo kwa uwajibikaji tanzania. kwa mara nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake wamefanikiwa kuwaingiza mkenge watanzania wakiongozwa na wapizani. Nani alitegemea kuwa wangerudia upuuzi wa Richmond ambapo serikali ilipaswa kufurushwa lakini ikamtoa waziri wake mkuu kafara na kunusurika huku wakubwa zake wakiendelea kupunga madili mengine? Katika kashfa ya escrow serikali na CCM wameshinda kile waingereza huita to win big. Wameweza kutoa kafara ya kuku (mawaziri) badala ya  mbuzi (waziri mkuu) ili kumnusuru ng'ombe yaani rais. Hivyo, KIDUMU CHAMA CHA MAFISADI. Na UFISADI unaendelea kama kawa. Tuombe Mungu aingilie kati kama alivyoonyesha kwenye gonjwa walilokuwa wakificha hivi karibuni ambapo rais amekiri kuwa anasumbuliwa na kansa ya kizazi. Tuombe Mungu atusaidie kuwafyeka majambazi wetu wenye ulaji. Amin.

Lesson learned from Chinese ivory saga

 
          Though it may be taken as a mere scandal, allegations that the president of China’s jet carried tons if not hundreds of kilos tarnished our image. Again, when did it begin? Boozers have some answers to this imbroglio. They urge that instead of blaming others we should blame ourselves first. Why? Because the way we've been doing things creates many loophole for our “foes” full of jealousy as Ben Membe put it.
 You know what. If there’s a person we need to blame first is none other than mzee Mchonga who said that ikulu’s been turned into a den of thieves. Interestingly, when mzee Mchonga made such allegations nobody repudiated. This means. Things are not well. How could they deny while what’s been going on is but sacrilege. Look at how they ruthlessly and carelessly spend our dosh on their oft-globetrotting. Do they care about boozers whose dosh they abuse? Go tell it to the birds if you think they do.
Why boozers say we’re the ones to blame? They know many things we either know and ignore or pretend not to want to know. They said openly and loudly that our ikulu needs to be checked. Who doesn't know that boozers are sick and tired of complaining about the tendency of concealing the names of the guys accompanying our big to his oft-trips abroad? Why are they concealing the names as if those accompanying the ding are not supposed to?
Another point, our “enemies” know how our hunk sits on scandals. Tell me. What happened to hoo-has of retrieving our dosh stashed in offshore and foreign banks? Have we forgotten how our chief Counsel Judge Freddie We-rema threatened to kick Swiss emissary, Olivier Chave out the hunk shall he keep on making noises about dosh stashed in his hunk? What else do you want to be tarnished? Do you know what happened to the suspects? Some were appointed to write a new constitution that boozers call constipation due to blessing greed and constipation in the hunk.
Caesar once told his wife when she’s alleged of wrongdoings. He said unto her, “The wife of Caesar must be above suspicion.” Is our “wife of Caesar above suspicion? Are our “wives” of Caesar above suspicion really? How can they be if at all some of them run suspicious companies aka NGOs? How can they be while others were suspected to transport our vipusa to Asian countries? Boozers still remember how Abdi Kinamna the top of Chama Cha Maulaji (CCM) was appointed amidst allegations. Why’s he appointed if at all we didn't look for being tarnished?
You know what. Boozers know how one topmost biggie’s suspected to be behind EPA profligacy. The dude’s nary repudiated nor defended himself. Was he behind EPA scam or not depends on how you look at things especially the code of silence and circumstantial evidence. If you want to know more as to why we’re the target of scams ask yourself what’s been done vis-à-vis Escrew dosh that’s recently stolen by IpTL and its affiliates. When Kafulia tried to sound the alarm he’s threated to be beheaded. As he persisted he’s called a monkey. Do you think this is in vain? Go hang if you do.
These “liars” who blew biggies’ cover say that when the current regime ascended to ulaji the hunk had over 140,000 jumbos. As of today, only 55,000 are left. Where did the missing number go? Do you think it is difficult to smuggle illicit items out of Bongo? If you do, you’re bewitched. Have you forgotten tons and tons of drugs that were impounded in Bondeni? How did they pass through our airport? If this doesn't convince you, look at this. Do you remember how many live animals were illegally transported to Meso East through KIA on November 26, 2010?  How many culprits were brought to book? Zero. What was done essentially is to just fire Obeid Mbangwa and other two people and that’s that. Why didn't they bring these criminals to book? Who knows?
Let’s look at the lesson learned from the saga in question. Firstly, it opened boozers’ eyes that not all that glitters is gold. You know what I mean. Secondly, it taught boozers the lesson that they’d try what Burkinabe tried just recently shall they deserve to live like bin-Adams but not the horses and beasts of burden they are today.
Thirdly, the big lesson from the saga is, we are doomed. Why if the holy of the holy is blessing such crimes. Our suspects need to come clean on this matter otherwise they've proved to be sitting ducks and connivers in the robbing of our God-blessed hunk. Don’t think I am becoming insincere and indifferent. Nay, I’m trying to devise the solution premised on what boozers think should be done.
Again, should we blame our foes for our embarrassment or just blame ourselves for our myopia, megalomania and gluttony?  Had this transpired in civilized hunk, the whole outfit’d have been pulled down. Again, who’ll do that in Bongolalaland aka Danganyika?

So long
Source: Guardian Tanzania. 

Mlevi kuwa-Compaore waliotu-escrow


                   Jambazi Blaise Compaore aka Ebola alipotaka kubadili katiba ili agombee mara nyingine kinyume cha sheria, walevi wa Burkina Faso hawakumkawiza zaidi ya kumdondosha. Hebu fikiria. Kama angekuwa amefanya madudu kama vile ku-escrow au ku-IpTL wangemfanyaje kama siyo kumchoma moto kama kibaka? Je hawa jamaa wangekuwa kayani mambo yangekuwaje? Kwa wasiojua maana ya escrow ni excessive stupidity committed repeatedly on Walevi. Na IpTL ni Interdependent political Thugs and Liars.
          Najaribu kufikiri kilevi na kibangi bangi ingawa nina hoja. Inashangaza kuona walevi wa njuluku wanavyotutendea kana kwamba sisi ni hamnazo. Jamani tuna akili hata kama tu walevi na wavuta bangi. Bila akili unadhani unaweza kuvuta bangi au kulewa na kusurvive usawa huu wa kila jambazi kujihomolea utadhani kaya yetu ni shamba la bibi? Yaani majizi inatu-screw nasi tunaendelea kufurahi utadhani hatuna hisia wala akili! Hapana. This is too much, inatosha. Lazima walevi tuwakomboe kondoo wa Mchonga wanaokubali kupelekwa majilini kirahisi na mafisi na machunaji ya kila aina kuanzia ya kisiasa na kidini.
          Walianza na HEPA, tukaminya. Waliona haitoshi wakaongeza Richmonduli. Tuliminya ingawa tulimbanjua mmoja. Waliona inafaa na wamefanya vyema. Sasa wanataka kufunga kazi na escrow. Kweli kuna haja ya kuwavumilia mchwa na mafisi kama hawa kweli?
          Najaribu kufikiri zaidi kilevi. Hivi kama tutatumia bongo vizuri, watuhumiwa wa escrew kweli ni hawa watano au wote? Huwezi kushughulikia escrow bila kugusa mama yake yaani IpTL ambayo ni alpha na omega mbele ya lisirikali letu linaloigwaya kama Ebola. Je kweli linaigwaya au wakubwa wake ni washirika wazuri wa IpTL? Ngoja nifundishe historia kilevi na kibangibangi. Je wajua kuwa IpTL iliingizwa na hawa hawa wanaojifanya hayawahusu huku wakitanua ughaibu wakisukuti jinsi ya kuwatoa kafara wenzao?
          Nakumbuka kila kitu utadhani kilitokea jana. Uzuri ni kwamba wakati wezi hawa wakiingiza balaa hili nilikuwa bado sijaanza kuvuta bangi wala kunywa kama sina akili nzuri. Nakumbuka mheshimiwa Njaa Kaya alikuwa waziri wa Nishati Mimaji na Midini by then.  Nakumbuka jinsi mzee Ruksa alivyotoa ruksa kwa wizi huu wa mchana simply because wapembe wake walikuwa wamepewa chao na kumwingiza mkenge wasijue wanazamisha kaya nzima.
          Turejee kule Burkina. Kwa vile hawa jamaa wanaonekana hawana uwezo wa kusoma alama za nyakati, basi mlevi napanga kuwaingiza walevi wote mitaani ili kieleweke. Sasa nitafanyaje iwapo wapingaji nao wanaonekana kuwa lezi lezi? Maana kwa wafwadhili walivyoshupalia hii kitu, kama atatokea mrume akaweka watu kwa mtaa dude lote litaporomoka kama Compaore. Mko wapi wapingaji au nanyi ni woga na washirika wa siri wa huu u-escrow na u-IpTL? Hivi mnashindwa nini kupiga la mgambo kuwaita walevi waende warejeshe heshima yao kwa kuwatimua hata kuwachoma moto mibaka?
          Sijui walevi wanachelea au kungoja nini wakati sababu ya kufanya kweli ipo na ni zaidi ya sababu? Wakati walevi wakilaza damu, utawasikia wakilalamika utadhani hawana akili wala sababu ya kufanya kweli. Acheni upuuzi. Amkeni tuwa-Compaore hawa waliotu-screw. Wamezidi kutugeuza mabunga na shamba la bibi.  Je mnangoja waishiwa wafanye kazi hiyo wakati uzoefu unaonyesha watachukua mbuzi wawili watatu wa shughuli na mchezo unaendelea?  Hata hivyo waishiwa wanabidi wawe makini kipindi hiki hasa ikizingatiwa kuwa mwakani wanakwenda kutafuta kura ya kula tena. Ili kuwaridhisha walevi wanapaswa wafanye kweli angalau wapate sababu za kuwaeleza walevi jinsi walivyowapigania na kuwaondoa kwenye makucha ya manyang’au mafisi na mafisadi.
          Je kuna haja ya kuwaachia waishiwa kila kitu wakati sisi tuna nguvu kuliko wao na hata ndata na ndutu na mitutu yao kama tutaamua? Mwenzenu nilikuwa Ouaga wiki mbili zilizopita. Nimeyaona na kuyashiriki yote na kugundua siri nyingi za kufanikisha kitu kitakatifu kama hiki hasa usawa huu ambapo ICC iko macho.
          Kwanini walevi tusiungane tukachoma shamba zima la ujambazi badala ya kuwaachia waishiwa wakate matawi huku wakiacha shina mbegu na mizizi kuzalisha matawi mengine? Hawa jamaa bila ku-Compaorewa hawawezi kupata somo. Wataendelea kujifanya kamchezo kama walivyozoea hasa wakijua kuwa walevi nao ni sawa na vibogoyo kiakili na kimsimamo. Kwa vile wote wanaonekana kujifanya haya mauzauza hayawahusu, basi Mlevi lazima niwape tafu wafwadhili kuhakikisha tunaangusha hili genge ambalo halina maana.
          Ifahamike kuwa kama nitafanikiwa kutimiza kuleta ukombozi wa walevi sifanya uzembe kama uliotokea Burkina ambapo ndutu walipoka ulaji na kujifanya ndiyo waliomuangusha Compaore wakati lao ni moja. Hata kayani kama nitafanikiwa nitahakikisha hakuna cha ndata wala ndutu kujifanya wao ndiyo wanajua kutawala wakati mambo yalipoharibika walichangia kuwalinda washenzi na mafisadi.

          Nimalizie kwa kuwaalika wote wenye uzalendo, visheni, usafi na usongo na kaya wajiunge nami kuingia mitaani kuwa-Compaore waliotu-screw chini ya ujambazi wa Escrow. Naomba kutoa hoja.
Chanzo:Nipashe

Saturday 29 November 2014

Laiti wote tungeona madudu ya Kikwete hivi!

Kikwete hawezi kushindwa yote hata pozi kwenye dege bovu la bei mbaya ambapo walipiga pesa kama escrow

Friday 28 November 2014

Imekaaje hiii escrow screw

Barua ya wazi kwa wabunge wote


Waheshimiwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano,
Bila kujali itikadi au mafungamano yenu, kwanza nawasalimu kwa jina la ukombozi wa taifa hili.
Pili nawasiliana nanyi kwa njia hii ili kuweza kuwashauri mambo mawili matatu kama raia na mzalendo wa taifa hili. Najua ugumu wa hali mnayokabiliana nayo kwa sasa mnapoelekea kwenye uchaguzi mwakani. Kwa wale wa chama tawala, najua fika mko msambweni hasa wakati huu mnapopaswa kuchagua kati ya taifa na chama.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake wamo msambweni. Wanakabiliwa na kashfa ya escrow ambapo inahusiana na wizi wa  takriban shilingi bilioni 200 hadi 300 zilichotwa  na baadhi ya watendaji mafisi na mafisadi toka wkenye akaunti ya escrow Benki Kuu. Hili halikubaliki. Hili ni kosa la jinai linalopaswa kushughulikiwa kwa kuwashughulikia watuhumiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni. Pia hili ni dhambi hasa kwa taifa maskini linaloishi kwa kutegemea kuombaomba na kukopa kopa ingawa baadhi ya wakubwa zetu hawaoni hili zaidi ya kuiba kufuja na kutumbua fedha ya umma maskini.
Hivyo, nawaombeni msome barua hii mkitanguliza uzalendo zaidi ya mafungamano ya kisiasa, kujuana, maslahi binafsi au kulindana. Kashfa ya escrow si ya kwanza kwa taifa letu. Zimepita kashfa nyingine nyingi kama vile EPA, Meremeta, SUKITA, uuzaji wa kijambazi wa mashirika ya umma na utoroshaji wa fedha nje. Muhimu niwakumbushe. Hii si mara ya kwanza kwenu, kama wawakilishi wa wananchi, kukumbana na hali kama hii. Nani mara hii anaweza kusahau ujasiri na uzalendo wenu mliposhughulikia kashfa ya Richmond ambapo mlimlazimisha waziri mkuu na mshirika wa rais mwenye ushawishi na nguvu Edward Lowassa kutema madaraka na ulaji akiwa anavitaka? Lowassa aliondoka akilalamika kuwa hakutendewa haki. Aliona kama ametolewa kafara. Hii maana yake ni kwamba watuhumiwa walikuwa ni zaidi ya Lowassa. Watuhumiwa walikuwa serikali nzima ambayo kwa bahati mbaya hamkuigusa. Mlijiridhisha kwa kuangusha mbuyu mkasahau kuwa mlisaza mingine mingi na mikubwa kiasi cha kutoa fursa ya kurudia mchezo ule ule kwa staili ile  ile. Sasa msikubali kufanya kazi nusu nusu wala kuridhishwa na kuangusha mibuyu miwili mitatu. Fyeka shamba zima lililogeuza nchi yetu kuwa shamba la bibi. Tumechoshwa na kashfa na serikali inayozishiriki badala ya kupambana nazo. Msikubali kugeuzwa mihuri ya kubariki na kuhalalisha jinai ya wizi na uhujumu wa taifa. Kuna kesho na kesho kutwa.
Hata hivyo, wapo wanaoona, pamoja na kazi pevu na adhimu, hamkuangalia chanzo cha tatizo. Hivyo, milishughulikia tawi na kuacha shina na mizizi ya tatizo. Sitaki nionekane nawafundisha kazi au kuwalaumu. Huenda hii ilisababishwa na taarifa mlizopewa pamoja na uzoefu. Kwani kashfa ya Richmond ilikuwa ya kwanza na ya aina yake kuwapambanisha na mihimili mingine.
Kutokana na uzoefu wenu hasa mkijikumbusha mapungufu yaliyotokea wakati wa kushughulikia kashfa ya Richmond, naamini kipindi hiki mtakwenda ndani zaidi na kushughulikia majani, matawi, shina mizizi hata mbegu ya tatizo mnalopambana nalo kama wawakilishi wa watanzania maskini wanaowamini na kuwategemea muwatendee haki.
Niseme wazi. Kashfa ya escrow ni zaidi ya watuhumiwa ambao ni mawaziri Profesa Sospiter Mungo na Saada Mkuya, gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndullu, Mwanasheria mkuu wa serikali jaji Fredrick Werema katibu wa wazira Eliakim Maswi na mkurugunzi wa Tanesco Felchesmi Mramba . Kashfa hii ni kashfa ya serikali nzima. Hivyo, kama mtadhamiria na kutaka kutenda haki, basi serikali nzima iwajibishwe. Tumesikia fununu kuwa kuna mpango wa kumtoa sadaka waziri mkuu Mizengo Pinda. Je Pinda anatolewa kafara kama nani iwapo wenye serikali wapo na wamekuwa kimya bila kutoa angalau tamko hata miongozo ya jinsi ya kulielekea hili?
Tumewasikia baadhi ya wakubwa wa CCM wakihanikiza mtende haki. Hawa wanasema hivyo ima kuwahadaa kuona kama hawahusiki au kwa kutojua ukubwa wa tatizo au kwa kujua lakini wakatumia janja hii waonekana wanakerwa na ufisadi.
Kumekuwapo na malalamiko mengi toka kwa wananchi wakilaumu hata wabunge wa CCM kuwa nao ni mafisadi. Sasa wakati wa kuwaonyesha wale wanaowatuhumu kwa vile ni wanachama wa CCM ni huu. Wakati wa kusafisha nafasi na nafsi zenu (hasa wabunge wa CCM) ni sasa. Itakuwa jambo la ajabu kama mtatishwa au kuwekwa sawa wakati mkijua fika mnayeweza kumuogopa (rais) anamaliza muda wake na haruhusiwi kugombea kisheria. Hivyo, wenye kuwa msambweni hapa si wengine bali nyinyi wabunge.
Mkienda mbali mkaaangalia hata hawa watuhumiwa, nusu yao ni wateuliwa wasio na imani wala kura ya wananchi. Hivyo, huu mtihani na mzigo wa serikali na chama msikubali kutwishwa nyinyi. Wananchi ni zaidi ya serikali na chama. Tanzania ni zaidi ya chama na serikali. Maisha ya kisiasa si karata bali utendaji. Hata kama tukiyaita karata, mnayo karata kipindi hiki. Msiliangushe taifa wala nyinyi binafsi.
Tumalizie kwa kuwaomba na kuwashauri kuwa badala ya kuhangaika na watuhumiwa wachache ambao kimsingi, ni wateule wa rais na washirika wa kundi kubwa la ufisadi zaidi ya hili, shughulikieni serikali nzima ili angalau muweke historia  ya kuleta ukombozi kupitia uwakilishi wenu. Tusingependa lawama mlizopata tokana na mchango wenu kwenye kuandika katiba mpya ambayo inaonekana wazi kutokuwa ya wananchi ziendelee. Wakati wa kuzifuta na kuwaonyesha wananchi kuwa bado mnawafaa na mnafaa kuchaguliwa tena ni sasa. Hata hivyo, si kwamba nawatisha. Mtakavyomaliza kashfa hii ndiko kutakakoamua hatima yenu kwenye uchaguzi ujao.

Niwatakieni kazi njema, afya tele na mafanikio katika mtihani huu wa kuonyesha au vinginevyo uzalendo au usaliti kwa taifa. SAA YA UKOMBOZI WA KWELI NA KAMILI NI SASA. Mungu ibariki Tanzania. Mungu bariki Bunge letu tukufu. Mungu wabariki wabunge na uwape visheni, maono, ujasiri, uzalendo na ukakamavu. AMINA.
Chanzo: Dira ya Mtanzania

Wednesday 26 November 2014

IPTL: Nani awajibishwe kati ya Pinda na Kikwete?


Mengi yameishaandikwa na kusemwa kuhusiana na kashfa ya wizi wa fedha za umma toka Benki Kuu (BoT) chini ya mfuko wa Escrow. Kashfa hii licha ya kunakera, inachefua, ni aghali, imegharimu taifa heshima, uaminifu, uwajibikaji, muda na fedha hata maendeleo. Imetuacha uchi na wa hovyo ukiachia mbali umaskini. Hivyo, katika kuishughulikia, wenye dhamana ya kufanya hivyo waende mbali kwa kuangalia historia nzima ya kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na jinsi ilivyoingizwa nchini kwa makusudi mazima ya kuliibia na kulihujumu taifa. Ifahamike, kashfa hii ni zaidi ya Escrow na watuhumiwa ambao wengi wamekamiwa kudondoshwa.
Kashfa ya Escrow, licha ya kufichua uchafu, uroho, ufisi, ufisadi, upogo, upofu, roho mbaya na jinai ya baadhi ya wakubwa zetu, imefichua utegemezi na uhovyo wetu na mfumo fisadi na zandiki. Licha ya kuhujumu na kudhalilisha taifa, kashfa hii, imelifedhesha hasa ikizingatiwa, kuna njama za kuizima wakitaka kutumia majaji, tuseme majanki, yaliyoteuliwa na wanaopaswa kubebeshwa zigo zima. Hapa ndipo uhovyo wetu kama taifa unagundulika. Kitendo hiki cha kutaka kuiua kashfa ya Escrow kimefanya wafadhili watudharau na kuamua kuingilia kati baada ya kuona hatufanyi mambo sawa sawa. Hii ni aibu na kilio kwa taifa. Je tufanyeje zaidi ya kujifunza kubadilika na kufanya mambo kama watu wenye akili timamu na uzalendo? Changamoto sasa iko mikononi mwa bunge letu tukufu ambalo si mara ya kwanza kukumbana na mtihani kama huu. Tunawaamini na kuwategemea wabunge wetu bila kujali itikadi, vyama au mafungamano. Taifa ni zaidi ya vyama na itikadi. Mtashinda tu mkidhamiria.
Wakati vichwa vikiuma juu ya namna ya kushughulikia kashfa hii, tunapaswa kujua chanzo cha sakata zima. Kwa mujibu wa historia ya kampuni nyonyaji na kidhabi ya IPTL, kampuni hii ilipata tenda ya kuzalisha umeme kwa taifa kwenye mazingira ya kutatanisha chini ya utawala wa Ali Hassan Mwinyi mwaka 1994 wakati rais wa sasa Jakaya Kikwete akiwa waziri wa Maji, Nishati na Madini kabla ya kuhamishiwa wizara ya fedha mwaka huo huo. Hivyo, unapoongelea IPTL huwezi kumaliza bila kuwataja Mwinyi na Kikwete. Mwingine aliyesaidia sana kuingizwa kwa IPTL nchini ni katibu mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) marehemu Horace Kolimba.
Hivyo, kushughulikia kashfa ya Escrow bila kuwagusa Mwinyi, Kikwete na wengine waliohusika kwa kiwango kikubwa kuhalalisha wizi kwa taifa jambo ambalo licha ya kusababisha ulanguzi na mgao wa umeme, sasa linatumika kuliibia taifa kijingajinga ni kupoteza muda na kukubali kafara.
Inashangaza kuona tunaposhughulikia wizi huu wa mabilioni kwa taifa maskini, anayeonekana kujua undani wa IPTL na mwenye serikali yake, yaani Kikwete, haguswi wala kuhusishwa. Wengi, kwa sasa, wamehanikiza kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda anaweza “kwenda na maji” kama Edward Lowassa aliyeenguliwa na kashfa nyingine kama hii ya Richmond. Je ni halali kuongelea au kushughulikia IPTL bila kumshughulikia walioiingiza na wenye kuonekana kujua mengi kuliko Pinda? Je hao watuhumiwa waliteuliwa na nani na walifanya kazi kwa niaba ya nani zaidi ya rais?
Wapo wanaoona kama historia itarejea na tabia ya kujirudia. Kama wenye dhamana ya kushughulikia kashfa hii, yaani wabunge, hawatakuwa makini, kuna uwezekano kilichotokea Februari 7, 2008 kujirudia ndani ya muda mfupi. Na ikitokea hivyo, tutakuwa tumepoteza fursa muhimu ya kutatua tatizo.Na kama ikitokea hivi, tutakuwa tumeshughulikia kafara badala ya mwenye dhambi anayetoa hiyo kafara. Tutakuwa tumekata matawi na kuacha mzizi wa tatizo ambao ni Kikwete, CCM na serikali nzima. Hivyo, kumaliza kadhia hii ni kushughulikia kiini kizima cha gonjwa badala ya matokeo.
 Kwa wanaokumbuka malalamiko ya Lowassa kuwa rais Jakaya Kikwete alijua kila kitu kuhusiana na Richmond, hawana shaka kuwa Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda, kama atatolewa kafara na bunge likaingia mkenge na kukubali, atarudia maneno yale yale. Je tutakuwa tumetatua tatizo au kumuacha wahusika wakuu kuendelee kucheza ngoma ile ile, kulihujumu taifa na kufanya kile waingereza huita, to get away with murder?
Tusingetegemea wabunge wapoteze muda kushughulikia vijidagaa na makuwadi wakati wenye mradi mzima wapo wakiendelea kufikiria jinsi ya kutenda madudu mengine. Hivi ni woga au ujinga? Bunge linaogopa nini kufumua mfumo mzima hasa baada ya kumtaka rais ajitetee hasa ikizingatiwa kuwa jinai hii imetendeka chini ya uangalizi wake ukiachia mbali kuwa sehemu ya historia ya tatizo? Muda wenyewe uliobaki kwenda kwa wananchi ni mdogo tu.
 Wakati wabunge wakitafakari haya wanapaswa kujiuliza swali moja: Je nchi hii ni mali ya nani zaidi ya watanzania bila kujali ukubwa wa nyadhifa zao? Je nani yuko juu ya sheria akaruhusiwa kutenda jinai atakavyo asishughulikiwe? Je imekuwaje serikali izembee na kukaa kimya hadi wafadhili waingilie kati kwa kuondoa fedha zao zipatazo shilingi zaidi ya trilioni moja wanazochangia kwenye bajeti ya taifa letu ombaomba na tegemezi lakini bado likawa na mshipa wa kuvumilia ujambazi kama huu wa Escrow na jinai ambayo imefanyika kwa muongo mzima ya IPTL na ulanguzi na mgao wa umeme ukiachia mbali uchafuzi wa mazingira tokana na kutumia teknolojia ya zamani kuzalisha nishati? Wakati haya yakiendelea, tunaambiwa deni la taifa linaumka bila maelezo ya msingi na bado tuna mshipa wa kuwavumilia wanaotenda jinai hii wakiongezea na ya Escrow na nyingine nyingi! Basi tu viumbe wa hovyo na wa ajabu kidogo.
          Tumalizie kwa kuwataka wabunge waende mbali bila kuangalia maslahi binafsi au kuogopa cheo cha mtu ambacho kimsingi ni dhamana toka kwa watanzania hawa hawa wanaohujumiwa na kufanyiwa ujambazi mchana kweupe.
Chanzo: Tanzania Daima leo.

Kijiwe chalaani majanki yaitwayo majaji

Baada ya mhishimiwa mmoja ambaye ametokea kuwa mpenzi na shabiki wa kijiwe kututonya kuwa matwahuti ya lisirikali na Chama Cha Mafisi na Mafisadi (CCMM) wanasuka mbinu ya kutumia mapilato kuzuia kijiwe cha Idodomya kisijadili na kufumua kashfa ya ujambazi wa kijinga wa Esrew, kimeamua kuwalaani na kutoa onyo.
          Msomi Mkatatamaa ndiye anayeanzisha mdaharo wa leo. Anakunywa kahawa yake na kutafuna mic, “Waheshimiwa maprofesa madaktari na maguru wa elimu wa kijiwe hiki mna taarifa kuwa kuna matwahuti wanataka kuua mjadala wa kashfa ya esrew kule Idodomya?”
          Mpemba anajibu, “Yakhe mie hayo nimesikia magazetini. Hivi kweli hawa waheshimiwa wetu waweza kubali fanyiwa ushenzi kama huu watumika kama mihuri ya kuhalalisha haramu hii?”
          Msomi hangoji mwingine ale mic. Anakwanyua mic, “Basi wasomi, taarifa nilizopewa na mhishimiwa Davie Kafulia ambaye ametokea kuwa shabiki na mpenzi wa kijiwe hiki kitukufu ni kwamba kuna mpango wa kutumia baadhi ya majanki yaitwayo majaji kuzuia mjadala ili kuepuka walioko nyuma ya jinai hii wasijulike wala kusulubiwa.”
          Mgosi Machungi anadandia mic na kusema, “Msomi huu ni upuuzi. Mbona tinawajua wote walioiba hii njuuku kwa sura na majina?”
          Msomi anajibu, “Nadhani hamuwajui wote.”
          Kapende anadandia mic, “Msomi hapa umeniacha hoi. Eti hawa majambazi wa esrew hatuwajui? Unamaanisha nini Msomi?”
          Msomi analazimika kurejea , “Najua mnawajua baadhi yaani wale watano yaani prof Sossie Muongo, prof Benny Ndururu, Saidia Mkuyati, Mura Freddie We-rema, Aliar Kim Maaswi na Filisinchi Muramba. Je ni hao tu?” anamalizia kwa swali.
          Wanakijiwe wanatoa mimacho bila kujua waseme nini. Ndiposa Mijjinga anaamua kutia guu, “Kweli usemayo profesa emeritus Msomi mwenyewe. Nadhani kama tutafanya uchambuzi yakinifu na wa kina synthesis na analysis, tutagundua kuwa wanaopaswa kubanwa na kupewa kichapo kwenye kashfa ya escrew siyo hao uliowataja wala mzee Mizengwe Pinder. Wapo akina Jimmy Rugemalayer na ponjoro Singa Herbinger of lot.”
          Msomi anachomekea, “Hata wewe bado huwajui. Maana unaotaja ni makuwadi na dagaa wanaotumiwa na papa na nyangumi mwenyewe.”
          “Yakhe wamaanishani hapa uniposema papa na nyangumi?” Mpemba anauliza kwa kuudhika kidogo.
Msomi anajibu, “Kwani esrew ni kashfa ya nani kama siyo IpTL ambayo ililetwa makusudi kayani kuibia wachovu? Unajua walioingiza hili balaa hadi wafadhili wakachetuka?”
Baada ya kuona hakuna anayejibu, Msomi anaendelea, “Someni au tafuteni historia ya usaliti huu mtagundua kuwa uliingia chini ya utawala holela wa ruksia huku mzito Njaa Kaya akiwa waziri Nishati, Midini na Mimaji. Kwa taarifa yenu waliosuka dili zima ni mkulu, Milima ya Kigoma, Horasi Kolimbae, Endelea Chenga, Joni Mhavi-le, Bill Shija aliyerejesha namba hivi karibuni , Abdi Kigodae,Dan son of Jonah, Meri Ndosssi, Raph Moreli na Jimmy Rugemalayer. Hata hawa si wote.”
Kapende hangoji, anakamua mic, “Kweli hatuwajui. Duh! Kweli kaya hii inabunguliwa na hawa mchwa bila huruma. Ukiwaona utadhani wanadamu kumbe mafisi na mchwa wa kutisha!”
Sofi Lion aka Kanungaembe anaonekana kuudhika wazi wazi. Anatia guu, “Watu wengine kwa kutoa madai mazito bila ushahidi wanakera. Hivi unaweza kutupa ushahidi wa haya yote unayozusha?”
Msomi anamchomekea Sofi, “Da Sofi kwanza futa kauli yako kusema eti nazusha. Tatizo la wachovu ni kutojisomea. Mbona taarifa za huu uchafu ziko kila mahali. They are all over the place.”
Sofi anaonekana kushikwa pabaya. Hajibu. Kanji kuona hivyo anajitahidi kuingilia kati kumuokoa mshikaji wake. Anasema, “Sasa kama shahidi iko all owa the place kwanini bunge hapana shughulikia vote nafanya hii mbaya?”
Mheshimwa Bwege anaamua kutia daruga, “Si kwamba wahishimiwa wameshindwa kushughulikia hawa manyang’au wala si kwamba hawawajui. Wanajua kila kitu. Wapeni muda muone kama hatawafanya zaidi ya walichofanya walipoingizwa mkenge na akina Sam Sixx na kumtoa kafara Eddie Luwasha. Taarifa nilizo nazo toka ndani ni kwamba haponi mtu hata huyu mkulu anayejificha kwa Joji Kichaka akidai anauguza busha.”
Kijiwe hakina mbavu jinsi anavyokandia.
Mijjinga aliyekuwa akibofya kisimu chake anaamua kuuma mic, “Kwanza nakupongeza Prof Emeritus Msomi mwenyewe kwa kuweka mambo hadharani. Ni kweli. Hiki kinachoitwa screw ni zaidi ya hapo. Hapa lazima CCMM, lisirikali na Njaa Kaya mwenyewe wapigwe chini ili tujikomboe na kuanza upya vinginevyo wahishimiwa wakubali kugeuzwa waishiwa kwa kupania vidagaa wakati mapapa na nyangumi yakiendelea kukata maji na kusababisha madhara zaidi hasa kwenye ngwe hii ya lala salama.”
Anakunywa kahawa yake na kuendelea, “Kwa tunaojua chesi zima ni kwamba njuluku hii imeibwa ili kuelekezwa kwenye uchakachuaji mwakani. Hata huyu Luwasha mnayesema alitolea kafara yumo mzima mzima. Maana wanataka kumjengea mazingira kuwa alionewa na pia anakubalika kwa kutumia utafutaji mlo unaoitwa utafiti. Kwani hamjui!”
Mzee Maneno anaamua kula mic, “Yote tisa. Nilicheka pale niliposikia kuwa kuna baadhi ya majanki yanataka kutumiwa kuzima moto huu yasijue yanaongeza mafuta. Nadhani sasa mnaweza kuona ukweli na mantiki ya kupinga kwetu uteuzi wa kishikaji na kulipana fadhila. Maana tuna majanki mengi yaitwayo majaji yaliyoteuliwa si kwa sifa wala kufaa bali uchafu na ushikaji wao.”
Kijiwe kikiwa kinanoga si lakipita shangingi la janki moja! Wacha tulitimue ili tulivue ujaji!
 Chanzo: Tanzania Daima leo.
 
 

Monday 24 November 2014

Who wants educated MPs?

Knowing how our hunk doesn't need sophisticated mortals --- it is hard to rule and bulldoze even dupe them--- Constitution Assembly (CA) otherwise known as Constipation Assembly came up with a very ingenious way of saving illiterates. Guess what. CA proposed that the qualification for becoming a Member of Mjengoni aka MP should be just standard seven certificate. If anything, this is but sounding death knell for our education which is already in ICU.
Many boozers didn't want to hear this. Again, who wants enlightened MPs who can query some deals in the house? Given that our hunk is heading back to pre-Adamic era, who wants bibliophiles whose education’s always caused us quandaries. I think this is why the minister for Knowledge and Skills Dr. Shchool Kawadog’s always  pushed our education down to the drain knowingly that we don’t need educated leaders. Again, who’s to blame since the hunk went to pooches? Top dogs have always been there to watch as if it doesn't concern them. Why should they bother if at all their vitegemezi are studying abroad?
If one’d ask boozers what the qualifications for becoming an MP should be, I’m sure. They’d say that kanywaji and bangi should too be considered to qualify for being an MP. To do justice for all, boozers think that even the president should know only how to write and read. Given that presidency is but ceremonial role of representing boozers, the president should be the guy who can smile and talk a lot but not the one who can listen and become serious in anything. Boozers want someone to please and make them happy. Thus, degrees and whatnot are not that important.
By proposing that the qualification for becoming an MP should be a Primary School Certificate, preferably obtained by being taught by UPE teachers, CA wants to discourage our biggies from forging their academic qualifications which has been going on unabated.
When CA proposed its qualification for becoming an MP, one boozer left us in stitches. He said that other qualifications should be:
Having many nyumba ndogo, big mouth and small ears, being a bachelor and among others being able to promise anything even if you don’t intend to live up to your words. However, one boozer came with a very different approach vis-à-vis MPs’ qualifications. He wanted them to have at least one undergrad degree in law so that they might be able to enact better laws as opposed to the current ones. He added that given that forging is no longer a crime, MPs must have PhDs that they’ll forge or bribe some university to award them honorary degrees. It is nice to have MPs with PhDs even if they didn't toil for them. Who wants to toil in the hunk where hard work doesn't pay?
By having Standard Seven Leavers in the house, we’ll be able to utilize our national language exhaustively. We’ll get rid of colonial languages which complicate things for many of our MPs. So too, we’ll abolish Kiswanglish which make boozers uncomfortable when oft-used by MPs who’d like to be regarded as educated even though they aren't.
If Swahili is going to be used, our farmers and boozers will understand what’s discussed in the mjengo as opposed to the current sideshows where Kiswanglish dominates the house. Also, by using national language, we’ll encourage dumb MPs to stop taking naps in the house. Instead, they’ll be able to contribute to the motions with confidence. I’m pretty sure my friends such as Joni Kombha and Stevi Wahasira won’t shuteye Mjengoni anymore. I treasured their photos taken when they were snoozing Mjengoni. They’re striking to look at. They show how our hunk is tolerant almost on everything. Had it been in western countries, napping Mjengoni would guarantee being kicked out right away without even waiting for voters to do so. If our hunk can allow a highly paid person to nap why can’t allow a person with little education that can’t enable even a sommelier to get a job? What else do we need? Are we looking for rocket scientists of just politicians who can tell us whatever they like? We need the guy who can tell us sweet lies of better life for everybody which means them but not us. Does lying need higher education really? When it comes to telling lies, I see no border between egghead and blockhead or illiterates. Importantly, beware and warned.  If you think: Education is expensive just try ignorance.
Source: The Guardian

Friday 21 November 2014

Mlevi afanya utafiti kuhusu uchaguzi ujao

Baada ya kuona wengine wakija na matokeo ya utafiti wao ambao wapinzani wao wameyaita mazingaombwe waliyopachika jina la utafiti wakati ni utafutaji mlo toka kwa mafisadi wanaotaka kugombea urais kayani, Mlevi ameamua kuja na utafiti wa kisayansi bila kujali kama ataitwa kihiyo anayejidai msomi. Wala sitajali kuitwa mchumia tumbo ingawa kweli kuna wachumia tumbo wanaoweza kutumia utafiti kusaka njuluku.
Hivyo, ufuatao ni utafiti uliofanywa na Mlevi usiolenga kusaka mlo wala kumpromoti yeyote. Kwa vile Mlevi ana shahada ya uzamivu Takwimu (PhD in Statics) aliyoipata kwenye chuo cha Hazard, huko kwa Joji Kichaka ameamua kuja na namna bora na ya kisayansi ya kufanya utafiti bila kubeba ngurumbili wala fisadi yeyote.
TWENDE KAZINI
Kupima kiwango cha uungwaji mkono kwa baadhi ya vyama vya siasa kayani hasa kulingana na usafi au uchafu na uwezo wao kuikwamua kaya toka kwenye mikono ya mafisi na mafisadi wanaokula kwa miguu na mikono bila kunawa huku wakipasiana.
Katika utafiti huu tulitafiti vyama kama taasisi zinazotoa wagombea badala ya watu binafsi. Maana, wahenga wanasema akili zenye rutuba hujadili masuala wakati zile zenye utapiamlo hujadili watu.
ZANA ZA UTAFITI
Yalitumika mahojiano yasiyo rasmi kwa njia ya simu za kiganjani ambapo waliopiga simu walikuwa na hiari ya kushiriki au kutoshiriki hasa baada ya kuambiwa haki zao kitafiti na kimaadili na si kimadili kama wale ambao wameficha hata waliogharimia utafutaji ulaji wao.
Mantiki ya utafiti ilikuwa ni kuangalia ni chama gani kingeweza kuchaguliwa kama uchaguzi ungefanyika sasa ili kuweza kuwajuza walevi anayefaa au wanaoafaa kuchaguliwa kwenye uchaguzi ujao.
HISTORIA YA KAYA NA UTAMADUNI
Tokana na kukithiri kwa uchakachuaji,wizi wa kura na hila mbali mbali za kutaka kuwapitisha mafisadi wagombee, nimeamua kufanya utafiti wa kisomi utakaowawezesha walevi kukataa kubambikiwa mafisadi wala kuibiwa kura  kwenye uchaguzi ujao. Hivyo, utafiti huu si ule utafutaji mlo toka kwa yeyote awe safi au fisadi. Ni utafiti wa kisomi na kisayansi kweli kweli.
KANUNI YA UTAFITI
Kuchanganua takwimu kuonyesha ukubwa wa tatizo la kuchakachua na kuiba kura ni mkubwa kayani ambapo mamlaka zinazosimamia uchaguzi ni zile zilitoteuliwa na wezi wa kura wenyewe huku ndata wakitumia kubeba chama twawala ili kiendelee kuwala walevi.
SAMPLI
Katika utafiti huu tumetumia aina ya mahojiano yajulikanyo kitaalamu kama snowball kwa kuhoji walevi 100 wanaume 50 wanawake 50 ambao walikuwa wa umri kati ya miaka 18 hadi 70 ambapo 70% walikuwa ni umri kati ya miaka 18-50 na 30% wa umri kati ya miaka 51 hadi 70.
Waliohojiwa walikuwa na kiwango cha elimu kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu ambapo 52% walikuwa na elimu ya kati ya shule ya msingi na sekondari wakati 30% ni kiwango cha High school hadi Diploma na 10% walikuwa na shahada ya kwanza na waliobaki yaani 8% walikuwa na shahada ya uzamili hadi uzamivu.
Utafiti umefanyika kwa miezi sita mfululizo ukihusisha mikoa yote ya kaya ya walevi.Uchambuzi wa takwimu Baada ya kufanya utafiti, tulichambua na kuainisha takwimu zilizoandikwa na zile zilizorekodiwa na kufanya mlinganisho na kuja matokeo ambayo nadhani kila mmoja analidhika nayo.
MASWALI YALIYOULIZWA
Kipaumbele cha uchaguzi ujao kiwe kurejesha rasmu ya katiba mpyai? Ndiyo au Hapana Vyama vyenye kashfa kubwa kama vile HEPA, Screw boozers, Richmonduli unadhani vizuiwe kushiriki uchaguzi? Ndiyo au hapana.
Kushindwa kushughulikia mafisadi hasa walioficha njuluku nje kutaangusha wale waliokuwa madarakani? Ndiyo au Hapana.Katika swali la kwanza waliojibu Ndiyo walikuwa watu 79 sawa na asilimia 79 ikilinganisha nwa waliosema hapana ambao walikuwa 21 sawa na asilimia 21.  Katika swali la pili waliojibu Ndiyo ni asilimia tisa ikilinganishwa na 10 waliojibu hapana.
Na katika swali la mwisho waliojibu ndiyo ni 95 ikilinganishwa na asilimia tano ambao bila shaka ni mafisi mafisadi au watu au watoto wao.Kwa ujumla walioonyesha uwezekano wa kushindwa chama twawala ni asilimia 88 ikilinganishwa na 12 ambao nao wanaonyesha hima kuwa mafisadi wenyewe au watu wao.Katika utafiti huu hapakuwa na rushwa wala hongo wala hatukuwa na mtu wetu kama wale wengine.
Utafiti huu uligharimiwa na walevi ili kupata taarifa safi zisizo za kupika wala kununua au kulenga kuvutia mafisadi fulani wakate pochi kama wale.Kwa ufupi ni kwamba utafiti huu umefuta uongo na hila vinavyoweza kufichwa kwenye utafiti kiasi cha kutoa matokeo yasiyowezekana kiakili.
Muhimu ni kuelewa kuwa hatukununuliwa, kushawishiwa wala kusaidiwa na yeyote katika utafiti huu adhimu. Ifahamike wazi. Wapiga kura hasa walevi na wavuta bangi wanapanga kuwapatiliza vidhabi na mafisadi wanaodhani wanaweza kutuungiza mkenge mwingine kwa kufanikiwa kujipenyeza au kupenyeza watu wao kwenye ikulu.
Walevi wanaonyesha kupenda vyama vyenye ajenda ya kupambana na ufisadi huku vikiamuru rasimu ya jaji Joseph Warioba irejeshwe ugani ili mawazo ya wananchi yajadiliwe na kuandika katiba safi.
By the way, tumegundua kuwa hali ya mambo kama uchaguzi utafanyika leo ni tofauti na tafiti nyingine zilizotangulia ambazo hata hivyo hazikutaja jinsi zilivyofanyika na nani walizifadhili. Hivyo, tunawashauri walevi wote kuupa utafiti huu umuhimu na kipaumbele. Kwa vile umekidhi viwango vyote vya kitafiti na kitaaluma, uwazi na ukweli. Tunatoa onyo hili hasa ikizingatiwa kuwa siku hizi uganganjaa imegeuka enterprise kubwa ambapo majambazi na mafisadi hutumia utafiti kupenyeza hoja zao.
Tukipata fursa tutafanya utafiti kuhusiana na mabilionea wa kweli.
Dondoo: Huwezi kuwa mhishimiwa aliyeko mjengoni kulinda maslahi ya baba yako na jamii yenu au kuwa mwizi wa Kagodamn ukawa bilionea. Utakuwaje bilionea atokanaye na kuibia umma, kukwepa kodi, kupunja waajiri wako mishahara na kufanya biashara haramu?
Tukutune wiki ijayo kwa mambo mengine yajayo. Onyo, watu wa Uwanja wa Ndege tafadhali acha mchezo wa kuruhusu miunga na vipusa kupitishwa hapo. Pia punguzeni rushwa. Maana wengi ni matajiri wa kutupwa tokana na kuendekeza njaa na rushwa. 
CHANZO: NIPASHE 

Please join me in praising Jah Almighty

Kwa wanaokumbuka hii ngoma nadhani watakuwa wamepata kitu roho inataka hasa usawa huu ambapo sanaa imegeuka ubabaishaji mtupu ukiachia mbali magwiji kuzidi kulala. Japo huu wimbo si wa The Gladiator bali Angola Maseko, bado una ladha na mulua. Nakumbuka miaka 90 kwenye maduka yangu ya kanda Mitaa ya Msimbazi na Kipata al maarufu Nkwazi Music Centres wateja wakija na kusema, "Tunaomba ile kanda ya maras wanaonung'unika sana."

Thursday 20 November 2014

Hii kitu mwaionaje?

Nimemkumbuka gwiji West Nkosi

Wapenzi wa penny Whistle ungana nami kumukumbuka marehemu West Nkosi (MPBH) kwa kibao hiki mulua.

Wednesday 19 November 2014

Visa vya marais wetu kutibiwa na kufia nje

 http://3.bp.blogspot.com/-sekbUKX_kb8/VGlok5rdW7I/AAAAAAAGxsg/ssF0x0qrcS4/s1600/0L7C0440.jpg
TAARIFA kuwa Rais Jakaya Kikwete amefanyiwa upasuaji wa tezi dume au busha (Prostate) bila shaka zilistua wengi kama si wote. Wengi hawakujua, ama walifichwa ukweli kuwa Rais anaumwa.
Hawajui ukubwa wa tatizo wala lilipoanza. Wanashangaa Rais kufanyiwa upasuaji. Kwani inaonyesha alishachekiwa na kugundulika ana tatizo. Hivyo, kufanya ahadi na mtaalamu wake aliyetajwa kama Dk. Edward Shaefer wa John Hopkins University, Maryland, Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa na ofisi yake, ni kwamba Rais anasumbuliwa na kinachoonekana kuwa kansa ya kizazi. Kwa jinsi taarifa zilivyotolewa kwa uchache, uwezekano wa mengi kusemwa ni mkubwa. Hata hivyo,  sitashangaa kusikia mengi hasa ikizingatiwa kuwa viongozi wetu huficha maradhi kana kwamba wao si binadamu wanaougua hata kufa.
Kuumwa ni kitu cha kawaida kwa mwanadamu ila kwa watawala wetu ambao wanajiona si wanadamu hii si saizi yao hadi yawakute ya kuwakuta. Tulidhani wangejifunza tokana na kifo cha baba wa taifa, Mwl Julius Nyerere ambaye wasaidizi wake waliufanya ugonjwa wake na kuufanya siri kubwa bila sababu zozote za msingi. Je watawala wetu na wapambe na waramba viatu wao watajifunza lini kuwa wawazi na wakweli?
Hivi karibuni taifa jirani la Zambia lilimpoteza Rais wake, marehemu Michael Chilufya Sata baada ya kuficha ugonjwa wake kwa muda mrefu hata kufikia kutishia kuwafunga wale walioonyesha shaka juu ya afya yake.
Mficha maradhi kilio humfichua. Kwani muda haukupita mauti yakafichua walichokuwa wakificha wenzetu wa Zambia.  Kuhusu taarifa za Kikwete kufanyiwa upasuaji ni ukweli kuwa inashangaza kuwa watanzania hadi sasa hawajui ungonjwa anaoumwa ni upi na ulianza au kugundulika lini na wapi.
Kwanini wanatuficha hivi wakati mhusika ni kiongozi wetu anayetibiwa kwa kodi zetu? Kukoleza mambo taarifa zenyewe zimetolewa kwa lugha nyepesi bila kueleza hata historia ya masahibu yake.
Hata hivyo, tunamtakia siha njema. Apone haraka ila tunawalaumu wasaidizi wake kuficha ugonjwa. Tusingeomba haya yaikute Tanzania. Maana, kwa wanaojua historia ya ziara za mara kwa mara za Kikwete nje, inaaweza kujengeka dhana kuwa alikuwa anaumwa kwa muda mrefu. Wapo wanaoamini kuwa ziara za Kikwete huku na kule ni kupambana na gonjwa ambalo hataki kuliweka wazi.
Pamoja na kuwa stahiki yake kutibiwa popote, wengi wanahoji ni lini watawala wetu wataimarisha huduma za afya nchini ili watibiwe hata kufia nyumbani? Wamehujumu na kuvuruga huduma za jamii.
Wanapougua, hata kutaka kupima mafua, hukimbilia Ulaya. Huu ni ubinafsi hata kama unatendwa na wakubwa. Tunapoandika Muhimbili ni nusu kaputi kihuduma. Nani mara hii kasahau kashfa ya hivi karibuni ambayo nayo imefutikwa chini ya busati ya chuo cha International Medical and Technology University (IMTU) kutupa mabaki ya miili ya binadamu kwenye mashimo ya kuchimba mchanga baada ya incinerator ya Muhimbili kuharibika kwa muda mrefu?
Nani hajui kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametuhumiwa kusambaza na kuuza madawa feki kama alivyofichuliwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida?
Je, amechukuliwa hatua gani zaidi ya kukingiwa kifua na wenzake wanaokimbilia Ulaya kupima mafua na kuacha watanzania waendelee kuteketea kwa magonjwa yanayoweza kuzuilika na kutibiwa nyumbani?
Je, Kikwete aligunduliwa lini na tatizo lake la tezi dume? Je, ahadi ya kukutana na mtaalamu (daktari wake) iliwekwa lini? Je, tatizo la Kikwete lina ukubwa gani? Haya ni maswali yanayojirudia sana.
Kuna haja ya kuweka wazi historia ya tatizo la Kikwete ili wananchi wajue. Kwanini walipie gharama zote za matibabu ya Rais wakati wamefichwa kinachomsibu? Rais si mtu binafsi kiasi cha kuficha hali yake ya kiafya. Kuendelea kuficha maradhi ya Rais si kumtendea haki wala watu wake.
Tunadhani wakati wa watawala wetu kubadilika na kututendea haki kama watu wenye akili sawa sawa umefika.  Kitendo cha kuendelea kukimbilia kutibiwa na kuangaliwa afya zao nje tena wakifanya siri kinawafichua kama watu wasiofaa kuwa viongozi.      Kinaonyesha walivyoshindwa vibaya sana na wapo madarakani kwa manufaa binafsi. Haiwezekani kila mwaka viongozi wa Afrika waletwe maiti toka nje. Je, Afrika itajitegemea lini?
 Hata hivyo, nchi ya Afrika Kusini imeonyesha mfano mzuri. Rejea jinsi baba wa taifa lile, Mzee Nelson Mandela alivyofia nchini mwake. Huu ni mfano wa kuigwa na ni suto kubwa tu kwa watawala wetu wanaojiangalia wao wenyewe na familia na marafiki zao huku umma ukiendelea kuteketea. Haya ndiyo maisha bora aliyowaahidi watanzania Kikwete? Kwanini roho zao haziwasuti kwa tabia hii ya mauaji ya halaiki barani Afrika?
Kuna haja ya watanzania kushinikiza walioficha maradhi ya Rais wawajibishwe mara moja ili liwe somo kwa wengine watakaofuata. Maana tumechoshwa na tabia hii ya kutawaliwa na miungu watu isiyougua wala kustahiki kutibiwa nyumbani.
Wanachofanya ni sawa na mama ntilie mmoja aliyepika chakula akawauzia wateja huku akiagiza chakula chake hotelini. Mama ntilie wa namna hii ni wa kususwa na kusitishwa kutoa huduma kwa umma. Maana hana udhu wala utu wa kuweza kufanya hivyo.
Chanzo: Tanzania Daima leo.

Kijiwe chajadili IpTL

 
BAADA ya kushuhudia hila, ghilba, minyukano na mizengwe kuhusiana na sakata zima la wizi wa fedha ya wachovu chini ya kashfa ya Esrew uliofanywa na baadhi ya wanene wasiogusika, Kijiwe kimeamua kujadili kadhia hii ili kutoa mapendekezo ya nini kifanyike.  Leo wanakijiwe wote tumerauka kweli kweli kuhakikisha tunatongoa na kutoa mchango kwa kaya yetu inayozidi kuangamizwa na mchwawatu na fisifisadi watu.
  Mpemba analianzisha, “Yakhe mmesikia hii mizengweee na nyimboo za hawa matwahuti wa Boko Haram ya kule Idodomya wanioendelea zungusha hili zali la IpTL?” anachomekea Mbwamwitu.
  “Unashangaa mizengwe ya Boko Haram wa Idodomya badala ya hili la mkulu kwenda kupasuliwa ughaibuni wakati hili laweza kufanyika hapa? Ami uwe na adabu. Utawezaje kuongea bila kutoa lau salamu kwa mkuu kwa kufanyiwa upasuaji wa busha?” Kapende anamtania Ami.”
“Hayo ya kupasuana mabusha mie hayanihusu. Yatanihusuje iwapo yangu hayawahusu hadi wenda nje kutumbua njuluku zetu kwa vijigonjwa viwezavyotibiwa hata Manzese?” Anauliza Mpemba kwa kuhudhika kidogo.
  “Mie kana kuna kitu kinanisumbua si kingine bai wizi wa Eskoo ambapo njuuku zetu zinazidi kuibiwa huku tikiona wavujaji wakienda kuganguliwa huko majuu wakati sisi tikiangamia kwa magonjwa yanayoweza kuzuiika na kutibiwa.” Anazoza Mgosi Machungi ambaye alipewa uprofesa hivi karibuni.
“Jamani mshaambiwa mali ya umma haiumi lazima uime. Ana shida gani wakati punda wa kuzalisha na kutoa njuluku kupitia kodi mpo kibao? Huyu kumbuka ni mfalme sawa na wale wa Uarabuni ambao huenda kutumbua Ulaya nyakati za mifungofungo” Anachomekea Mijjinga aliyekuja na tabu kubwa utadhani anakwenda chuo cha Manzese kuanza uprofesa wake wa kupewa.
  Mpemba anarejea, “Mie ndhani leo tuongelee hili la ujambazi wa IpTL badala ya kuongelea upuuzi mdogo mdogo kama vile mabusha. Sioni kama kupasua au kutoyapasua kwatusaidia kitu sie akina yakhe.”
  “Ami umenena vyema. Mabusha na kaya wapi na wapi. Naona tukumbushane kuwa kuna janga liitwalo IpTL-Escrow limtafuna kila mmoja wetu,” Msomi Mkatatamaa anazoza.
  Kabla ya kuendelea kudema Mgosi anamchomekea, “Hebu msomi tieewane. Unasema eti haya mazimwi yanatitafuna ukimaanisha nini? Kama kutafunwa watafunwe wae walioyaleta na kuendeea kuyakingia kifua lakini si Mgosi.”
  “Lisirikali litoe maelezo na baada ya hapo kuwawajibisha watendaji wake kwa kuwafikisha mahakamani baada ya kuwafilisi.” Mipawa anazoza kwa uchungu na ngoa.
 “Rugesingasinga na Harbinger of theft wakamatwe na kufilisiwa na wafie lupango ili liwe somo kwa wengine,” Anaongeza Mheshimiwa Bwege.
“Hivi mna ushahidi wa mnayosema au chuki na wivu ndivyo vinawasukuma kupayuka mnayopayuka?” Bi Sofi Lion aka Kanungaembe anaamua kuchafua hewa.
“Kwani wewe unao ushahidi wa haya unayosema?” Mchunguliaji anamuuliza Sofi kwa utani.
Kanji hakawii, “Kweli iko vatu iba juuku ya kaya lakini hapana dai yote. Mimi jua iko vatu dani ya lisirikali iba hii bilioni. Hii hindi kama natumiwa tu au naonewa. Mizi iko ofisini ya sirkali.”
“Hebu mwagia yeye sana. Maana Kanji iko toa pwenti kuba sana. Zengwe zima liitwalo IpTL litokomezewe mbali kwa kutamka wazi kuwa halitaruhusiwa kufanya shughuli yoyote kayani.” Mijjinga anampa ofa Kanji tokana na pwenti zake mulua.
Msomi anarejea, “Sheria zitungwe kuhakikisha kuwa hawa matapeli na mabwana wao kwenye lisirikali hawabadilishi jina na kuendelea kuula kama walivyofanya Richmonduli chini ya koti la Dowanis.”
Anabwia kahawa na kuendelea, “Nadhani wote ni kambale. Hao wakubwa tunaowalilia watende haki ndiyo wahusika wakuu. Mmesahau walivyotuibia kupitia EPA? Hapa la kufanya ni kupiga chini lisilikali la Chama Cha Mafisi na Mafisadi (CCMM) bila cha msalie mtume.”
“Wakigoma twende zetu Burkina Faso na kuwaonyesha kilichomnyima Compaore aka Ebola jeuri ya kung’ang’ania ulaji,” anababatiza Kapende.
“Mie naona ni kama tunatwanga maji. Kwanza tunapaswa kujua IpTL ni nani hawa badala ya kuzungwa na hawa mafisadi kuwadi wawili wanaotumikishwa na wenye mradi walioko nyuma ya pazia,” anachomekea Mipawa.
“Umesema vyema kwa vile IPTL ni zaidi ya Rugemalira na Ponjoro Singh. Ni serikali ndani ya serikali au vipi?” Mzee Maneno anaramba mic.
“Kwa wanavyozungusha, kuna namna. Sioni tofauti ya ujambazi huu na ule wa EPA ambapo mkulu mwenyewe alikamatika akashindwa hata kurukuta zaidi ya kujifanya hasikii wala kujua tuhuma.
Kwa wenye akili tunajua nini jambazi wa EPA sawa na hawa wa Esrew. In fact we have been screwed. Samahani namwanga kikameruni na kikwini aka kimombo tokana na hasira,” Msomi anazidi kuchanja mbuga,” Msomi anachukia hadi anamwaga ukameruni utadhani yuko London.
Mgosi anachomekea kwa utani, “Uongee na kishambaa kwa vie Mombo ni Ushoto kwai? Kama mbwai mbwai mbwa ale mbwa hapa.”
Kijiwe kikiwa kinanoga si likapita shangingi likiwa limewapakiza Sossie Muongo, Saada Mkuyati, Filiinchi Mramba, Ben Ndururu, A liar Kim Maswi, Jimmy Nshomile Rugesingasinga na Singa singa Harbinger of hell. Acha tulitimue kwa mawe tukitaka kulikamata na kuwachoma moto baada ya kuwanzia kitu mbaya ili kuondoa huu ujinga na usanii. Bahati yao dereva wao aliongeza mwendo na kutuacha na mimawe yetu.
Chanzo: Tanzania Daima leo.

Monday 17 November 2014

Kumbe na wanasiasa wanatapeliwa!


Askofu wa kujipachika wa dhehebu la Good News for All Ministry  Charles Gadi wa pili kulia pamoja na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi kwenye maombi ya kumwombea rais Jakaya Kikwete anayetibiwa nchini Marekani baada ya kupasuliwa busha (Picha kwa hisani ya IPPmedia).

Wanasiasa huwatapeli wananchi. Kadhalika nao hutapeliwa na waganga wa kienyeji na wachunaji waitwao wachungaji. Huu mchezo umeanza kuota mizizi ambapo unasikia matapeli eti wakiliombea taifa badala ya kuliambia kuwa linaharibiwa na hawa miungu watu wanaowaabudia ili wawape tenda na vijipesa kidogo au kujifanya hawaoni utapeli wanaofanya hadi wengi wametokea kuwa mabilionea hata wanaoweza kununua ndege.
Matapeli hawa kiroho kwa kujua kuwa watawala wetu ni wachafu, woga na wasiojiamini, wamewaingiza mjini kiasi cha kuwatumia kupata umaarufu na kuwaibia. Rais wa zamani wa Malawi alitumiwa vilivyo na tapeli la kinigeria TB Joshua ambaye hata hivyo utapeli wake ulipata pigo hivi karibuni pale nyumba yake ya kulala wageni ilipoporomoka na kuua zaidi ya watu 100 wengi wakitokea Afrika Kusini ambako tapeli huyu ana wafuasi wengi.


Uhuni dhidi ya Warioba mbona ikulu inajichanganya?

 
          Taarifa iliyotolewa na ikulu baada ya kuchelewa muda mrefu kuhusiana na sakata la kuvamiwa na kutaka kupigwa kwa waziri mkuu wa zamani Jaji Joseph Warioba, zinachekesha. Hivi Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, alikaririwa akisema, “Tumekerwa sana na tukio lile, halikutufurahisha hata kidogo kama Serikali kwa kuwa limemvunjia heshima Mzee Warioba, yule ni mzee wetu, anahitaji heshima, kwanza heshima yake na ulinzi.”
Je ni machozi ya mamba? Inakuwaje ikulu itoe tamko, kwanza ikiwa imechelewa? Na pili, baada ya mkuu wa ikulu yaani rais kutoa tamko akionyesha wazi kufurahishwa na yaliyomsibu Warioba? Je ikulu inamsemea nani wakati mwenye ikulu ameishajisemea. Kikwete alikaririwa akisema, “Nadhani na mimi nitakavyokuwa napiga kampeni hayatatokea yale ya jana (juzi), maana mie sioni haya kuipigia kampeni kama wale wenzetu ambao wanataka isipite.” Haya si maneno ya busara kwa kiongozi wa nchi tena akiongelea tukio la kupigwa kiongozi mwenzake tena mwenye uzalendo kuliko hata huo wake. Je maneno ya Kikwete hayaonyeshi kufurahia na kuridhishwa na uhuni aliofanyiwa Warioba. Je Kikwete alishindwa nini hata kumpa pole mzee Warioba hata kama ni kwa kuondoa laawama? Kitu kizuri alichofanya Kikwete ni ile hali ya kushindwa kuficha chuki yake dhidi ya Warioba na furaha yake kwa uhuni aliotendewa Warioba.
Tujalie kuwa kweli Ikulu imeudhiwa na kukerwa na yaliyomkuta mzee Warioba. Je nani mkweli kati ya Sefua na Kikwete kuhusiana na sakata hili? Je kwanini ikulu ilichelewa kutoa tamko kama hakuna namna? Je ikulu inadhani kuwa mzee Warioba na watanzania ni wajinga kiasi hiki na wasahaulifu kushindwa kupembua pumba na mbegu? Je jibu ni “kufedheheshwa’ au kuwachukulia hatua wahuni na wahalifu waliotaka kumzuru Warioba? Je ni wangapi wameishakamatwa? Je vurugu na udhalilishaji aliofanyiwa Warioba angefanyiwa Kikwete polisi wangekuwa bado wanasuasua?
Sefua alijinanga zaidi pale aliposema, “Najua si jambo zuri, iliwahi kutokea pia kwa Mzee (Ali Hassan) Mwinyi, alipigwa kibao... sasa kingine ni mazingira yanapotokea matukio haya, wakati mwingine ni ngumu.” Mbona kwenye sakata la kupigwa kibao mzee Mwinyi mhusika alikamatwa pale pale na kufikishwa kwenye vyombo vya dola? Je polisi wanaopaswa kuwalinda watanzania walikuwa wapi kama hakuna namna?
Kimsingi, watu kama Sefue na Mkurungezi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu walipaswa kuwajibishwa mara moja kwa kuonyesha kunyamazia uovu wakionyesha chuki na upendeleo vya wazi. Sijui tunajifunza nini kwenye matumizi ya upendeleo kisheria? Ndiyo ni upendeleo. Kwanini wahuni waliotaka kumdhuru Warioba hawakukamatwa siku hiyo na kufikishwa kwenye vyombo vya dola? Je hawa polisi ni wa nini wanaolipwa kodi zetu lakini wakatumia madaraka yao kwa upendeleo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na uonevu dhidi ya wale wasiokubaliana nacho kama mzee Warioba na wapinzani kwa ujumla?
Hii inakumbusha sakata lilolotekea siku chache kabla ya hili la kufanyiwa fujo mzee Warioba ambapo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Halima Mdee alitupwa korokoroni na kucheleweshewa kupewa dhamana ambayo ni haki yake kisheria wakati watuhumiwa wa makosa mbali mbali kama vile kusambaza na kuuza madawa feki yanayowakabili akina Ramadhani Madabida mwenyekiti wa CCM wakifumbiwa macho.
Polisi, ikulu na CCM hawawezi kukwepa lawama kwenye uhuni huu. Mbona polisi hao hao waliweza kwenda kwenye makazi ya mtu saa saba usiku huko Kyerwa kuzuia kufanyika mkutano wa CHADEMA uliokuwa umeishakubaliwa siku chache kabla ya kuja na tamko hili lenye kuonyesha machozi ya mamba ya wazi? Hapa lazima kuna namna na wananchi wasipoamka na kuchukua hatua, wataendelea kuumia na kuumizwa huku wakidhulumiwa haki zao kwenye nchi yao na kuishi kama wakimbizi kwenye nchi yao. Hii nchi ni yetu sote bila kujali itikadi wala mafungamano ya mtu. Kufungamana au kutofautiana na chama chochote ni haki ya watanzania kikatiba.
Kitendo cha ikulu ambayo siku chache kabla ya kuja na mazingaombwe ya  “kukerwa’ na uhuni aliofanyiwa Warioba iliwezaje kupata muda wa kutangaza kutenga mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kupigia kampeni katiba anayopinga Warioba kabla ya kutoa tamko? Kama kweli katiba inayofanya watu wadhalilishwe ni bora kama anavyosema Kikwete, mbona wanaoipinga wanafanyiwa uhuni na kuonekana kama hawana haki na uhuru wa kuipinga kama raia wengine?
Japo wanaofanya ujinga huu wa kushabikia uhuni wanaweza kudhani wanaawakomoa akina Warioba na wote wanaopinga katiba yao kiini macho, wafahamu. Wanamdhalilisha rais wao ambaye naye ameamua kujiingiza kwenye mambo yasiyolingana na hadhi yake. Huwezi kusema, “Nadhani na mimi nitakavyokuwa napiga kampeni hayatatokea yale ya jana” ukaeleweka wala kutenganishwa na watu wanaofurahia upuuzi huu. Nadhani kitu ambacho ikulu inaweza kufanya na kueleweka ni kukiri kuwa ilifurahia masahibu ya Warioba. Hivyo, imuombe yeye na umma wa watanzania msamaha kwa hili tuendelee na mambo mengine. Hebu tutoe mfano wa hivi karibuni. Rais Kikwete amefanyiwa operesheni ya tezi dume hivi karibuni huko Marekani. Hivi akitokea mtu akasema “natamani hili lisinikute’ wakati akiongelea afya ya rais mtamuelewaje? Tujalie Warioba au kiongozi yeyote wa upinzania aseme hivyo ikulu itamchukuliaje? Kwanini mkuki unakuwa halali kwa nguruwe na kwa binadamu mchungu? Unafiki ni wa nini katika shughuli za umma? Nani atakaa madarakani milele? Mbona mzee Mwinyi alifanyiwa uhuni na watu hawataki kujifunza? Ampigaye mzaziwe naye atapigwa na amkiaye mabaya mwenzie naye yatamkuta tena makubwa kuliko hayo.
Chanzo: Dira ya Mtanzania.