The Chant of Savant

Thursday 25 June 2015

Buriani Kamukara


Japo sikuwahi kukutana na marehemu Edson Kamukara uso kwa uso, tulifahamiana na kuongea sana karibu kila wiki kabla hajahama toka gazeti la Tanzania Daima.  Kamuraka ndiye aliyekuwa mhariri wangu katika gazeti la Tanzania akishughulika makala zangu mbili maarufu kama Kijiwe na Nyingine ambayo sijui waliipa jina gani.
Nikiwa najiandaa kulala, nilipitia kwenye mitandao japo kujua kilichojiri nyumbani. Kama kawaida huwa nasoma habari za huko hasa ikizingatiwa kuwa wakiamka tunalala na tukiamka wanajiandaa kwenda kulala. Hivyo, taarifa ya kifo cha Kamukara kilichotokana na moto wa jiko la mchina zimenichanganya kwa jinsi nilivyomjua kijana huyu ambaye alikuwa anaonyesha kuwa na bright future. Nimeona madhara ya mgao na umeme usio na uhakika umaskini na ushenzi mwingine vinavyoandama nchi za kiafrika. Ni bahati nzuri kuwa ni leo tu nilikuwa napitia kwa mara ya mwisho kitabu changu kipya cha AFRICA REUNITE OR PERISH ambapo masuala kama haya nimeyaongelea kwa undani zaidi.
 Kama nilivyodokeza hapo juu, sikumjua kwa sura japo tulijuana sana.
Kamukara alikuwa kijana si muaminifu tu bali mkweli na mstaarabu. Nakumbuka malipo yangu yakichelewa au kupunjwa tokana na makosa ya kiuhasibu alikuwa halali hadi anapata ufumbuzi. Kama hakuwa anacho anachojua aliweza kusema bila kuficha.
Kwa majonzi naona siwezi kuendelea. Ama kweli wema hawadumu.
NENDA SALAMA MAREHEME EDSON KAMUKARA
Mungu aiweke pema peponi roho yako.
Aaamiiiiiiiiiiiiiiiiiiinaaaaaaaaaaaa

1 comment:

Anonymous said...

Afya na usalama ni elimu itolewa katika vyombo vya habari na ikiwezekana kwenye mkusanyanyiko wa umma, vyama vya kijamii ili tuweze kupunguza ajali kama hizi. Mungu amlaze pema peponi Mpiganaji mwenzetu