The Chant of Savant

Tuesday 28 November 2017

How long will Arabs keep on discriminating against and selling Africans to slavery?

When animalistic europe started slave trade, nobody knows that it would take many years to stop. The first slave trade, according to scholars,saw over 12 million Africans being shipped to the Americas, Europe and Middle East to be used as slaves at home and in plantations.  After making a killing which enabled it to enter into what is historically known as Industrial Revolution,  Europe abolished slavery. Again, the couple in this business are known to be Arabs and Europeans.
              Since, it was abolished, slavery seems to have resurged recently when African or arabs pedigree in the modern maghreb started to sell Africans as slaves. The above clip can give you an inkling on what is now going on while the world, especially the so-called international community has kept mum simply because modern slaves are sold, restricted and sometimes die in the maghreb instead of crossing over to Europe. This is good for the holy europe that should not be invaded and disturbed by Black creatures.
       Many Africans are not fleeing conflicts and poverty in their countries which have Europe's hallmarks. Many African countries, mainly those endowed with resources, are facing violent conflict in which warlords start war so as to have control on resources they sell to the West.
           When it comes to poverty, bad governance, corruption and dependency, among others, are to blame. Many African countries are ruled by corrupt and inept regimes whose goals in power is exploiting their countries for narrow and personal gains. Interestingly, such rulers are supported by the same Europe and the west in general to see to it that they are perpetually colonised for the interests of Europe. The story is very complicated and long. Again, why have Africans always been welcoming their torturers? What would have been the reaction of the world had Africans sold their modern slave masters in the maghreb? Sheer hypocrisy and racism. 
    

4 comments:

Anonymous said...

Salaam Mwalimu Mhango,
Muda wa kudumu hakuna dini yoyote iliyopiga marufuku utumwa na biashara ya utumwa hususa dini ya Kiislamu waarabu wataendelea kuwafanya waafrika ni watumwa wakati wowote ule nafasi inapopatikana kwa sababu tu kwa Waisilamu kitabu chao ni kitabu cha kila zama na kila mahala.Kwa maana hiyo sheria zote ambazo zinazoendesha utumwa zipo hai na inategemea ni wakati gani na wapi,kwa hiyo kinachotokea Libya kitawashsngaza tu jamii zisizo za kiisilamu duniani lakini kwa waisilamu wenyewe ni jambo la kawaida kwa sababu tu kitabu chao sheria hizo bado zipo hai na zinafanya kazi.Ikiwa nci kama ya Mauritania hadi hii leo utumwa hupo hai,Saudi Arabia bado hupo hai na kuna Sheikh mmoja wa Sudani amepigia debe biashara hiyo ya utumwa ifufuliwe rasmi Sudani alipoulizwa watumwa hao watapatikana wapi alijibu kwa wepesi mno kwamba wapo tu kwa wingi South Sudani.
Kwa vitabu vya dini nyingine ambazo zimeukubali utumwa na utaratibu wake kijamii sheria hizo imebaki kama ni somo la historia tu katika dini au ni HERITAGE katika dini hizo,kamwe hazitofufuliliwa kiutekelezaji popote pale ampapo waumini wa dini hizo wanapatikana.Na tukumbuke tu kwambai ni nchi za kiisilamu ndio zilipinga na zilikwa za mwisho kukubaliana makubaliano ya kuharamisha utumwa na biashara ya utumwa.

Na kwa bahati mbaya Mwafrika ndio jinsi ya mwisho kufanywa mtumwa na kuchukuliwa utumwani nje ya bara lake na hakuna Jinai kubwa ilifanywa na Waarabu katika uovu wa uataratibu wa utumwa kama kuwahanisisha(castrate) watumwa wa kiume,na ndio maana tunaona hakuna ongezeko la waafrika katika nchi za kiarabu ambazo Waafrika walichukuliwa kama watumwa.Waarabu daima watamwangalia na kumzingatia Mwafrika kama ni mtumwa na mtu duni vyovyote vile iwavyo na mafano hai tumeuona kwa kudhalilishwa Rais Obama katika ziara yake ya mwisho ncini Saudi Arabiai.Na neno mtumwa(Abdu) katika lugha yao ya kiarabu ni sawa (synonymous) na Mwafrika.Nimalizie tu kwa kusema kwamba vyovyote vile tutavyolaani ushenzi huu na ukatili huu wa waarabu katika jinai hii ya utumwa katika karne hii ya 21 kwa waarabu(WAISILAMU) kwao wao bado wanaishi katika karne ya 7 ambayo walikuwa wakiishi na sheria na kanuni za utumwa na biashara yake kutokana na mafunzo ya dini yao.Na sio kinachokubaliwa na kubarikiwa kutoka mbinguni kinakuwa ni sahii wanadamu wenyewe tuna haki ya kukitaa na kukikemea na jinai hii ya utumwa umekubaliwa na kubarikiwa kutoka mbinguni kwetu itakuwa ni JINAI TU KATIKA HISTORIA YA MWANADMU NA UANADAMU.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...


Anon nakushukuru sana kwa mchango na mchanganuo wa kihistoria. Nakubaliana nawe kuwa dini zote mamboleo ambazo hupenda kuziita duni zilihalalisha utumwa na ubaguzi dhidi ya mtu mweusi na kuwa utumwa ni jinai dhidi ya utu. Unaposema AU iingilie kati unasahau kuwa kuna waswahili wenzetu kama vile wanyamwezi walishiriki kuwauza wenzetu. Hivyo, hao watawala wetu ni wanyamwezi wa kileo. Ni jukumu letu wahanga kuamka na kuamua kuionyesha dunia kuwa sisi ni watu japo binadamu kama wao. Mie ushauri wangu ni rahisi ķuwa tuanze kujihami kwa kuzikataa dini na itikadi zao huku tukizidisha kuelimisha watu wetu wajitambue waache kujibagua na waanze kujithamini na kuthaminiana. Insshangaza kusikia baadhi ya waislamu nchini kusikika wakilalamikua kuteswa kwa wenzao wa rohingya huko Myanmar lakini wako kimya dhidi ya udhalishaji na commodification ya mwafrika.
Wakati mwingine tunapaswa kujilaumu waswahili sisi wenyewe kwa kushindwa kusimama na kuonyesha kuwa nasi ni watu. Mfano, tumeridhia mfumo baguzi ambapo waarabu na wahindi hutubagua lakini huendelea kushirikiana nao badala ya kuwazira na kuwagomea. Imefikia mahali hata waswahili wenzetu kama vile wapemba, wasudani na wasomali eti nao wanatubagua na kututenga wakijiona wao ni waarabu zaidi ya waafrika wakati wakienda huko uarabuni wanakoabudia huitwa abid yaani matumwa. Ukienda Tanga utaona hili. Mazali a na masalia ya waarabu yanaruhusiwa kuoa mabinti wa kibantu lakini wao hawatuozeshi hata yale mazalia ya mazalia ya dada zetu. Kuna haja ya sisi waaafrika kujielimisha na kuelimishana juu ya nafasi yetu katika dunia. Kwa mfano, ukimgusa mhindi au mwarabu leo utasikia waislamu wakilalamika kuwa ni kwa vile ni muislam. Pia tupambana na dhana potofu kuwa ndugu wa muislamu ni muislam. Hata mbuzi na kuku pamoja na ubongo mdogo wanajua ndugu zao ni nani. Wakati mwingine tujilaumu. Kama washenzi hawa walikuja na dini na itikadi zao na kutubadilisha majina tukakubali kwanini wasiendelee kutudhalilisha hata baada ya kugundua kuwa walitufanyia kitu mbaya? Inabidi tuanza kuchunguzana na kushughulikiana pale tunapogundua kuwa kuna wenzetu wanaotaka kutuhujumu chini ya kisingizio chochote. Kawaida ukimnunua mbwa na kumfuga, lazima umpe jina jipya ili uweze kumtambua akiwa katikati ya mbwa wengine. Nidyo maana walitubadilisha majina na kutupa majina yao ya kishenzi. Siku moja niliweka makala hapa na video juu ya manma wahindi wanavyowatenza kama wanyama waswahili waliko kwenye kisiwa cha Andaman waitwao Jarawa. Sikuona waswahili wakichangia. Juzi dada yetu mtanzania alipigwa na kuchomewa gari India huku wahindi wakiwaita waafrika absii au kalu yaani manyani ndiyo viongozi wetu wanazidi kujivua nguo kuwakaribisha waje kuwekeza bila hata kuulizia kwanini wanwabagua watu wetu. Je namna hii wataacha kutubagua na hatimaye kutuuza? India wasingekuwa na tatizo la ongezeko la watu na ufukara, wangekuwa wa kwanza kutaka kununua watumwa wa kiswahili. Kwa wale wanaoona kutetea utumwa wao uitwao dini ni haki yao tuwashauri waende ima Makka au Roma wakafanye hivyo huku wakituachia afrika yetu. Tunajua ni lini tulikuwa waislam au wakristo lakini hatujui ni lini tulikuwa waafrika.

Anonymous said...

Salaam mwalimu Mhango,
Nami nakushukuru sana na nimekuwa nikikushukuru daima kwa kazi yako ya kupigania Bara letu la Afrika na waafrika kwa udhalimu wote uliotukuta unaotukuta na utakao endelea kutukuta.Umekuwa mwenye kuyatafuta maradhi yetu ya kijamii kuanzia jinsi ya kufikiri na jinsi ya kutenda na kuchukua maamuzi na kuyatafutia dawa na hali hii ndiyo wenzetu(thimkers) wa Ulaya walifanikiwa katika kutibu maradhi mbali mbali ya kijamii na kisiasa kwa kuyatafutia dawa stahiki na nilisema kwa wati fulani kwamba endelea na kazi yako hiyo hata kama kizazi hiki hakitokuelewa lakini kizazi kijacho watakuelewa tu kwa sababu ulikuwa ni shahidi wa zama zako.Lakini kwa wakati wetu huu bado utaonekana na kuchukuliwa kama Mpayukaji tu na unaota ndoto za machana lakini kwetu sisi ambao tunauona umuhimu wako kama prophet na witness kwa watu wako hatutokata na hatutakata tamaa na tutaendelea kukusoma na tutachangia maoni yetu kila tukipata wasaa.

Mwalimu Mhango,wache nianzie pale ulipomalizia katika jumla hii ulipoandika......"kwa wale wanaoona kwa kutetea utumwa wao uitwao dini ni haki yao tuwashauri waende imma Makkah au Roma wakafanye hivyo huku wakituachia afrika yetu.Tunajua ni lini tulikuwa waisialamu au wakristo lakini hatujui ni lini tulikuwa waafrika".Kwa maelezo haya hapa umegusa jeraha au donda ndugu katika akili ya kufikiri ya Mwafrika,japo umeweza kueleza jinsi gani jeraha hili au donda ndugu hili linaweza kutibika lakini kwa maoni yangu kwamba hata tukifanikiwa kutibika bado makovu yake yatakuwa yanaendelea kutuathiri daima.

Tatizo kubwa la mwafrika nikuendelea kuishi katika akili ya UTAMADUNI WA KITUMWA!!Utamaduni wa kitumwa Mwafrika huyu awe huru wa kiwiliwili 100% lakini atabaki kuwa ni mtumwa tu vyovyote vile awavyo,utamaduni wa kitumwa unaanza pale tu Mwafrika anapaanza kujikaa kama yeye ni mwafrika kwa sifa zote za uafrika na kuanza kuendelea kukumbatia kupigania na kuwa tayari kupoteza maisha yake kwa ajili ya dini,mila desturi na utamaduni wa wale ambao waliomsababishia madhara yote hayo ya kutojitambua kwamba yeye ni mwafrika.
Inaendelea..............

Anonymous said...



Mwalimu Mhango,umekuwa ukipiga makelele sana kuhusu waafrika kupoteza majina yao,kwangu mimi hili sio tatizo la kukera kwani ukiingalia kwa undani zaidi tukijiita na kupigania majina yetu ya kiafrika wakati hatuna ambacho cha kujidaia katika dini zetu mila,tamaduni na destruri zetu ni sawa na kuwa artificial golden vase ambalo halina thamani yoyote ile ya dhahabu halisi na hivi ndivyo tulivyo.Sasa hivi kuna mwamko sana kwetu Tanzania kwa watoto kupewa majina ya kiafrika bila ya kupandikizwa au kuelimishwa uafrika ni nini.Kuwa na jina la kiafrika au rangi nyeusi peke yake haitoshi kupigania uafrika ni lazima watu wapandikizwe kujidaia uafrika wao na hata kufikia hatua ya ubaguzi inapolazimika kutetea uafrika huo kama vile kuwabagua wahindi,waarabu na wa mfano wao pale tu wanapohatarisha indentity yetu ya kiafrika na hata masilahi yetu ya kijamii.Leo hii waisilamu wa Tanzania katika harusi zao kama hujaelewa kama ni watanzania kwa picha tu unaweza kuelewa kwa wepesi kabisa kwamba hii harusi ni ya watumwa weusi (waafrika) waliopo katika nchi ya Omani!!! na k2a ndugu zetu wa kikristo hali kadhalika uwezi kutofautisha harusi zao na zile ambazo zinazofanyika katika bara la ulaya au marekani.Kwa nini nchi za Afrika mgaharibi wafanikiwe katika mavazi na tushindwe sisi watanzania kama si kutawaliwa na utamaduni wa kitumwa?

Nikubaliane na wewe kabisa kwamba kama tutaweza kuiona dini ni kama swala la mtu binafsi linalomuhusu yeye na kile anachokiamini bila ya kuilazimisha dini yake kwa mtu mwingine au kuingiza katika siasa tunaweza kupiga hatua kwa afrtika tatizo ni dini kwani kwa uwoga wa kuogopa kuiuliza mbigu na wawakilishi wake ambao wanaodai wanaiwakilisha mbingu tatizo hili la utamaduni wa kitumwa bado utaendelea kuwa ni janga kwetu kwani inapotokea kuwa wasomi wetu kuwa ni sehemu ya tatizo na wala sio sehemu ya ufumbuzi safari yetu itakuwa ndefu katika kujikomboa na BALAA HILI LA UTAMADUNI WA KITUMWA.Hivi kweli Karl Marx hakuwa mkweli wa 100 % pale aliposema kwamba "Dini ni madaya ya kulevya kwa watu?"